Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Shirika la KIWOHEDE yaiitaka Jamii, serikali na wadau mbalimbali kushirikiana kwaajili ya kumlinda mtoto ili kuweza kutokomeza matendo ya ukatili ambayo yanatokana kwenye jamii.
Ushauri huo ulitolewa na Mratibu wa Mradi wa sauti ya wasichana, Arodia Aloyce wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya mtoto wa Afrika yaliyoanza leo yaliyofanyika Jijini Dar es Salama
Arodia amesema shirika hilo limeadhimisha siku hiyo kwa kutekeleza mradi wa kuimarisha nguvu ya sauti za wasichana kwa kutoa elimu katika vituo vyao salama ili kuhamasisha wazazi, watoto na vijana kupinga ukatili kwenye jamii.
Aidha Arodia amesema wametumia siku hiyo kwenda na vijana pamoja na watoto ambao wameshiriki kwenye michezo lakini pia wamefika na bidhaa ambazo wamezitengeneza kwa mikono yao.
“Kwa sisi kama KIWOHEDE tumeadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kuja na wasichana wetu ambao wametoka katika Wilaya nne ambao tumetengeneza nao mradi wetu wa kuimarisha nguvu ya sauti za wasichana ambapo Kauli mbiu ya siku ya mtoto wa Afrika ni ‘Tuimarishe ulinzi wa mtoto tokomeza ukatili dhidi yake, jiandae kuhesabiwa’ “
KIWOHEDE ni shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na watoto, vijana ambapo wanaishi katika mazingira hatarishi pamoja na wanawake ambalo Lilianza tangu Mwaka 1998 na kusajiliwa mwaka 1999, limalofanya kazi katika mikoa mbalimbali ikiwemo mbeya, Mwanza, Dar es Salaam, Iringa, Kigoma na singida
More Stories
Dkt.Tulia ashiriki ibada, asisitiza waumini kushiriki uchaguzi serikali za mitaa
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia