November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake watakiwa kuwania nafasi za uongozi

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Wito umetolewa Kwa wanawake kutoka maeneo mbalimbali kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi na kuachana na Mila potofu za kuona kuwa hawana uwezo

Hayo yameelezwa mapema Jana na Bi Anna wambura Kwa niaba ya spika wa bunge la Tanzania Dkt Tulia Ackson wakati akizungumza Jana katika mkutano wa kimataifa wa wabunge kutoka jumuiya ya wanawake wabunge wa kikanda na wadau wa masuala ya wanawake kutoka nchi za Afrika ulioandaliwa na Taasisi ya kimataifa ya uongozi demokrasia yenye usawa wa kijinsia Idea Lead Africa.

Wambura alibainisha kuwa ni muimu sana Kwa wanawake sasa kujitokeza Kwa wingi katika kuwania nafasi za uongozi hasa kwenye siasa Kwa kuwa uwezo wao ni mkubwa sana

“Sio tu wanawake wenyewe wajitokeze kuwania kama ambavyo nimewaambia bali hata ile Jamii inayomzunguka mwanamke wampe nafasi mwanamke “aliongeza

Wambura alieleza baadhi ya changamoto na vikwazo ambavyo zinavyomkwamisha mwanamke kutowania nafasi ya uongozi ni pamoja na majukumu ya kifamilia katika malezi pamoja na mila na desturi zinazowaonyesha kuwa wanawake ni kumbe duni.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa wabunge wanawake wa Bunge la Afrika mashariki,Fatuma Ndangiza alisema lengo la mkutano huo ni kuwapa kimpaumbele wanawake katika kubadilisha uzoefu wa masuala ya uongozi.

“Matarajio yetu baada ya majadiliano hayo tutaweka mikakati mbalimbali na kuwasilisha changamoto hizi katika mabunge yetu kama wawakilishi wa wananchi ili kuweza kubadilisha sera zinazowakwamisha wanawake wasifikie ngazi za maamuzi.

Mmoja wa wadau wanaopigania haki za binadamu kutoka Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo,Agnes Sadiki alisema ni vyema wakuu wa nchi anashukuru kukutana na wanawake kutoka nchi mbalimbali kwani itasaidia kuhamasisha wanawake kuwani uongozi mbalimbali na kuweza kufanya maamuzi.

“Tunaomba wakuu viongozi waliosaini mkataba katika kuwainua wanawake katika nafasi ya uongozi waweze kutekeleza na kwa upande wa wanawake waongeze juhudi katika kufikia ngazi za uongozi ili waweze kufikia hamsini kwa hamsini katika nafasi mbalimbali,alisema Sadiki.

Kwa Upande wake Sifisisami Dube ambaye ni Kiongozi wa IDEA LEAD Afrika amesema kwamba Taasisi hiyo ambayo inafanyakazi chini ya mwamvuli wa ubalozi wa Sweden ambapo wanalenga kazi tatu muhimu ikiwemo kusaidia masuala ya uchaguzi ushiriki wa kisiasa na kufanya masuala ya katiba katika nchi zinazohitaji kusaidiwa katika masuala hayo.

“Lakini hii wamejikita katika kitu kimoja ambacho ushiriki wa wanawake katika nyanja ya siasa pia Wana kipengele Cha vyombo vya habàri vinavyojihusisha katika ajenda mbalimbali ushikishwaji katika siasa” alihitimisha