November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jamii yaaswa kutowadharau  wanawake 

Na  Esther  Macha, Timesmajira,Online,Arusha

JAMII imetakiwa kuacha tabia ya kudharau wanawake kwa kuona kuwa hawafai kuongoza nafasi mbali mbali za uongozi na kusema kuwa wanawake wana uwezo wapewe nafasi za uongozi waweze kuwatumikia watanzania .

Imeelezwa kuwa kuna wanawake wana uwezo wa kufanya vitu mbalimbali vya kiuongozi mfano  nafasi mitaala shuleni kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi wanawake  katika kuwajengea uwezo wa kujiamini na kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuwania nafasi za kiungozi.

Akifungua mkutano wa siku tatu  ulioandaliwa  na  Taasisi ya Kimataifa  inayoshughulikia Demokrasia na Usaidizi wa Uchaguzi (IDEA)kwa kushirikiana Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA),Mbunge Anastazia Wambura kutoka Tanzania kwaniaba ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania,Dkt.Tulia Ackson alisema mkutano huo unalengo  la kujadili changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wanawake katika masuala ya uongozi.

Mbunge Wambura alisema endapo wanawake wakiwa viongozi wataweza kutatua changamoto mbalimbali za kiongozi,kisiasa na kijamii kwani wao wanabaini changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo ikiwemo malezi ya watoto na kuwa wanawake ni chombo kikubwa cha amani.

Aidha alitoa rai kwa jamii kuacha kuwaona wanawake kama ni viumbe duni wasiojiweza kutoa mawazo yao na kujadiliwa lakini uongozi wa kisiasa ni mzuri katika uongozi.

“Lazima sasa tujikwamue wenyewe katika kuwania nafasi mbalimbali za kiungozi na Tanzania tumepiga hatua kubwa Kwa kutoa Rais Mwanamke,Samia Hassan Suluhu na Spika wa Bunge Dkt,Tulia Ackson tuongeze idadi ya viongozi wanawake ili tuweze kutatua changamoto mbalimbali”

Alisema  majukumu mengi ya familia na kijamii yanapelekea wanawake wengi wenye uwezo wa kuongoza  kutojihusisha na masuala ya siasa badala yake kubaki kulea familia pekee.

Alisema endapo wanawake wakiwa viongozi wataweza kutatua changamoto mbalimbali za kiongozi,kisiasa na kijamii kwani wao wanabaini changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo ikiwemo malezi ya watoto na ni chombo kikubwa cha amani

Alitoa rai kwa jamii kuacha kuwaona wanawake kama ni viumbe duni wasioweza kutoa mawazo yao na kujadiliwa lakini uongozi wa kisiasa ni mzuri katika uongozi

“Lazima sasa tujikwamue wenyewe katika kuwania nafasi mbalimbali za kiungozi na Tanzania tumepiga hatua kubwa Kwa kutoa Rais Mwanamke,Samia Hassan Suluhu na Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson tuongeze idadi ya viongozi wanawake ili tuweza kutatua changamoto mbalimbali”

Naye Spika wa Bunge la EALA,Martin Ngoga alisisitiza kuwa haki za wanawake ni haki za binadamu wote hivyo jamii iwape haki sawa katika kuhakikisha hata wanapotoa michango yao maofisini,kisiasa na kijamii waheshimiwe kwani mwanamke ni kiongozi asiyetetereka

Naye Fatuma Ndagiza ambaye ni katibu wa Mkutano huo,alisema kuwa mfumo wa vyama vya siasa sio rafiki katika ngazi za uongozi ikiwemo wanawake kutopewa nafasi ya kujadili changamoto zao ikiwemo watoto wa kike hivyo ni vema wanawake wakapambania haki zao ili waweze kuongoza katika nafasi mbalimbali

Mzungumzaji kwa niaba ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anastazia Wambura
Pichani ni baadhi ya wabunge wa nchi za Afrika