November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Emirates yaingiza ndege mpya ya mizigo

Na Penina malundo,timesmajira,Dar es Salaam 

SHIRIKA la ndege la Emirates  SkyCargo ambayo ipo chini ya ndege ya Emirates ,imepokea ndege mpya ya Boeing 777 kutoka kampuni ya Boeing Paine Field ya nchini Marekani.

Taarifa iliyotolewa na Makamu wa Rais kitengo maalum wa Shirika la Emirates SkyCargo, Nabil Sultan, kwa vyombo vya habari na Shirika hilo la Ndege la Emirates amesema ndege hiyo inafanya kuwa jumla ya ndege zake 11 ambapo ndege ya Boeing 777 ni mahususi kwaajili ya kusafirisha mizigo pekee.

Amesema  kwa mara ya kwanza ndege hiyo imefanya safari yake kutoka nchini Marekani  kwenda Hong Kong kuchukuwa mzigo yake ya kwanza kabla na kuelekea nchini  Dubai.

“Ndege yetu mpya inaongeza kasi kwenye kazi zetu ambapo tulichapa kazi kwa bidii katika kipindi cha Corona na kuhakisha kwamba wateja wetu duniani kote hawakosi huduma,”amesema na kuongeza

“Tunatarajia kupokea ndege mpya nyingine mwezi huu aina hiyo hiyo,mwakani 2023 tutaaanza kubadirisha ndege nne za abiria aina ya 777 aircraft ziwe ndege za kusafirisha mzigo,”amesema

Amesema hali ya  uwekezaji unaonesha kwamba wako tayari kuwahudumu wateja wao na vifaa hodari kuhakisha mzigo ya muhimu inasafirisha bila tabu yoyote na biashara inafanyika vizuri
kupitia Dubai.

Amesema huduma ya Emirates SkyCargo inafika katika sehemu 11 duniani na kutoa huduma kwa wasafirishaji kwenye ndege za abiria, 200 za Boeing 777 na Airbus A380s ambayo zina fika katika maeneo   130 katika mabara sita.

“Kwa Mwaka jana, Emirates SkyCargo ilisafirisha takribani tani milioni 2.1
ya mizigo mbalimbali na itaendeleza safari zake kama moja wa wasafirishaji wakubwa duniani,”amesema