November 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya KCB yashiriki maadhimisho ya siku ya saratani

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Benki ya KCB imeiomba jamii kushirikiana kuhakikisha kansa inafutika pale panapowezekana lakini pia kuwasaidia wale ambao wamekumbwa na wanaopambana na ugonjwa huo kwa kutoa misaada mbalimbali.

Hayo yalisemwa leo (Juni 5, 2022) na Mkuu wa masoko wa Benki ya KCB, Christina manyenye wakati wa Maadhimisho ya siku ya mashujaa wa Saratani ambayo huadhimishwa kila Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa sita ambapo kwa mwaka huu yameadhimishwa katika Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar es salaam.

Mkuu huyo wa masoko amesema wao kama Benki ya KCB wameendelea kutoa misaada kwa watu wenye kansa katika hospitali mbalimbali ikiwemo Ocean Road kwa kutoa vifaa tiba lakini pia ukarabati wa majengo.

Manyenye amesema Mbali na kansa, Benki ya KCB imetoa misaada mingi kwa hospitali mbalimbali hapa Tanzania hasa kwa upande wa wakina mama (wodi ya wazazi) na watoto.

Aidha amesema ni jukumu la kila mtu kumuwezesha kijana mwenye kansa hasa kwa kumpa elimu na kumpitisha katika ujasiriamali;

“Benki ya KCB tunawasaidia wanawake na vijana ili waweze kuzintunza familia zao endapo watakutana na magonjwa Kama haya ya kansa au changamoto nyingine za kijamii”

“Kansa ni ugonjwa na kushughulika ili kuiondoa hii kansa ni kitu ambacho unaweza ukakiangalia kwa namna moja au kwa upana zaidi, kwa sisi KCB tumeona kwamba watu wanahitaji kuwezeshwa hivyo tunawezesha vijana kwa kuwapeleka wakasome mfano kwenye chuo cha ufundi (VETA) na kuwapitisha katika ujasiriamali na wengine kuanzisha biashara zao wenyewe lakini pia kuwapa mikopo nafuu”

Pia Manyenye amesema Changamoto kubwa ni watu kuogopa kupima kansa, lakini ni vyema ukiwahi kupima na kapata matibabu mapema.

Ameongeza kuwa katika vijana ambao wamewasaidia wa mwaka 2019 yupo mmoja ambaye alikutwa na kansa hivyo wao kama Benki ya KCB wanaangalia namna ya kumsaidia kijana huyo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa serikali, Dkt. Aifello Sichwale amesema nia ya siku hii ni kusherehekea mafaniko ya mashujaa waliowahi kuugua saratani lakini pia kuwapa moyo wale waliogundulika na saratani hivi karibu lakini pia kwa wanaoendelea na matibabu.

Dkt. sichwale amesema waathirika ni wengu wapo walioathirika moja kwa moja lakini pia wasioathirika moja kwa moja.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage ameishukuru serikali kupitia kitengo cha MSD kufanikisha upatikanaji wa dawa za tiba kemia ambapo kwa sasa zinapatikana kwa takribani 95%-98%

Kwa upande wake mmoja wa shujaa wa saratani amesema matibabu yanapatikana vizuri na muhimu watu wajitokeze wapate matibabu sahihi ambapo kwa Ocean Road yanapatikana kwa wakati.

Mkuu wa Masoko wa Benki ya KCB akipokea cheti kutoka kwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichalwe , kwa kutambua mchango wa Benki hiyo kusaidia mashujaa na wagonjwa ambao wanaendelea kupigana na ugonjwa huo, maadhimisho yalifanyika jana Jumapili Juni 5, 2022 Katika Hospitali ya Ocean Road, Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Masoko wa Benki ya KCB, Christina Manyenye akiwa katika matembezi ya amani wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mashujaa wa Kansa ambayo huadhimishwa kila Jumapili ya kwanza ya Mwezi wa Sita, Mwaka huu yamefanyika jana Jumapili Juni 6, 2022 katika Hospitali ya Ocean Road, Jijini Dar es salaam