Na David John, TimesMajira Online
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Anjelina Mabula amevitaka vyombo vya habari kusaidia kuibua na kuripoti habari zinazohusu changamoto kwenye sekta Ardhi kwalengo la kuisaidia Serikali kuharakisha wa kero zilizopo kwenye Sekta hiyo.
Dkt Mabula ametoa kauli hiyo leo Mei 4/6/ 2022 mkoani Dar es Salaam katika mkutano uliowakutanisha wahariri wa vyombo vya habari pamoja na waandishi ambapo amesema katika sekta ya ardhi kuna migogoro na changamoto mbalimbali hivyo niwajibu kwa vyombo vya habari kuibua kero hizo ili kutoa fursa kwa serikali kuweza kushughulikia.
Amesema kama inavyoelezwa kuwa vyombo habari ni muhimili wanne usio rasmi na wahariri pamoja na waandishi wahabari kupitia vyombo vyao watumie hiyo katika kutoa elimu na kuibua changamoto hizo.
Dkt .Mabula alizitaja moja ya changamoto ni migogoro ya ardh inayosababishwa na umiliki zaidi ya mmoja katika eneo moja .nyingine ni mashirika kushindwa kulipa madeni ya wizara yanayotokana na ardhi.
“Hivyo nichukuwe fursa hii kuwaomba ndugu zangu wahariri pamoja na waandishi wa habari kutumia fursa ya kikao hiki kwenda kuripoti habari nyingi zinazohusu changamoto zilizopo kwenye ardhi”Amesema Waziri Dkt. Mabula
Nakuongeza kuwa “nimategemeo yangu kuona baada ya kikao hiki nitaona na kusoma habari nyingi zinazohusu sekta ya ardhi iili kutoa nafasi ya kuzishughulikia sisi kama serikali na maofisa wangu wamejipanga kwa ajili ya kutatua “amesisitiza Waziri Dkt Mabula
Pia katika hatua nyingine amezungumzia mkakati uliopo ndani ya wizara ya ardhi hasa kwenda na kasi ya kidigitali ambayo ndio dunia iliko sasa nakwamba wao wamejipanga ili kuondoa kero na kupunguza migogoro dhidi ya wananchi kuweka taarifa zote kupitia mifumo ya kidigitali.
Amesema Rais Samia Hassan suluhu ametoa shilingi bilioni 50 ambazo zimekwenda katika Halmashuri 55 ili kuwezesha kupanga maeneo husika hivyo nivema vyombo vya habari kusaidia kuzungumzia changamoto zilizopo kwenye sekta ya ardhi.
Pia Waziri Mabula amesema kuwa wao kama wizara wamejipanga vizuri sana kupitia maofisa wake kwenda kuazisha Kiliniki za kutatua kero zilizopo kwenye sekta ya ardhi hapa nchini ambapo kiliniki hiyo itakwenda maeneo husika ili kutatua migogoro ya ardhi ambayo wanakabiliana nayo wananchi.
Katika hatua nyingine Waziri Dkt. Mabula akizungumzia madeni amesema kuwa wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inadai shilingili bilioni 78 kwa mashirika na umma na binafsi hizo zote ni changamoto ambazo vyombo vya habari zinamchango mkubwa wa kuzungumzia kwa maslahi mapana kwa maendeleo ya taifa letu.
More Stories
Dkt.Tulia ashiriki ibada, asisitiza waumini kushiriki uchaguzi serikali za mitaa
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia