Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Katika kuhakikisha watoto wanasoma kwenye mazingira mazuri zaidi ya milioni 154, zimechangwa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati kwa shule za msingi zilizopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Ambapo kiasi hicho kimepatikana katika hafla ya chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangia madawati kwa shule za msingi wilayani humo iliyofanyika jana Kata ya Nyasaka wilaya ya Ilemela kwa usimamizi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Massala na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Massala,ameeleza kuwa kabla ya kuwaita wadau kwa ajili ya kuchangia Wilaya kupitia Halmashauri ya Manispaa yake imetoa fedha za kumalizia majengo ya madarasa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi, kuongeza shule pamoja na madawati 1000.
Massala ameeleza kuwa changamoto iliyopo kwa sasa ni upungufu wa madawati 5830 ambayo yanahitajika katika shule za msingi zilizopo wilayani Ilemela.
“Uandikishaji wa shule za msingi umekuwa maradufu hali inayopelekea kuleta changamoto ya upungufu wa madawati ambapo katika darasa moja linalopaswa kuwa na wanafunzi 45 utakuta zaidi ya wanafunzi 150, tulihitaji madawati 6830 ila sisi kupitia Manispaa yetu tumetoa madawati 1000 hivyo yamesalia madawati 5830,”ameeleza Massala.
Aidha amewashukuru wadau wote waliochangia katika hafla hiyo ambayo jumla ya shilingi 154,910,000 zilipatikana huku akiwaalika kushiriki siku ya kukabidhi madawati hayo itakayofanyika Julai Mosi, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula,amesema serikali italeta mpango katika kutatua changamoto mbalimbali za kimaendeleo ila hawawezi kujua utaelekezwa sehemu ipi inaweza kuwa maabara, hosteli au kwa ajili ya walimu hivyo ametumia fursa hiyo kumpongeze Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuja na mpango na kuwa na maono pamoja na kuelekeza jitihada katika kutatua changamoto ya ukosefu wa madawati kwenye shule za msingi wilayani humo.
Dkt. Angeline ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kuchangia shughuli za maendeleo huku serikali itaendelea kuhakikisha inashirikiana na wadau hao ambapo katika kuunga mkono jitihada hizo amechangia jumla ya madawati 340.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amewaasa Wakuu wa Wilaya na viongozi wengine katika ngazi zao kuiga mfano wa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela jambo litakalosaidia kupunguza changamoto huku akichangia kiasi cha milioni 1.
Mhandisi Gabriel,alitumia fursa hiyo kumpongeze Mkuu huyo wa Wilaya kwa
maono yake na ubunifu wake kwa kuona pamoja na mapato ya ndani na changamoto za Wilaya lakini aliamua kuanza na suala la madawati ili wanafunzi waweze kukaa katika mazingira mazuri ya kusomea.
“Alichofanya Massala ni ufunguo kwa wakuu wa wilaya wengine kuleta ubunifu kama huu ili kuondoa changamoto za nchi,”amesema Mhandisi Gabriel
More Stories
Mwalimu adaiwa kumfanyia ukatili mwanafunzi
NAOT watakiwa kuendana na viwango vya ukaguzi
10 Best Online Internet Casinos For Real Cash Oct 202