Na Jackline Martin
Katika kuadhimisha siku ya Vipimo Duniani yenye kauli mbiu inayosema ‘Matumizi ya Vipo Kidigitali’, Wakala wa Vipimo Mkoa wa Ilala imetoa wito kwa wafanyabiashara kutumia vipimo vilivyo sahihi kwa njia ya kidigitali ili kuweza kurahisisha biashara zao na kuongeza thamani ya pesa kwenye shughuli zao za kilasiku.
Akizungumza wakati wa Maadhimisho hayo leo jijini Dar es Salaam ambayo huadhimishwa Kila tarehe 20 Mei ya Kila mwaka, Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA), Mkoa wa Ilala, Lilian Mwombeki amesema wao Kama Wakala wa Vipimo Mkoa wa Ilala wanatumia maadhimisho hayo kutoa elimu kwa wafanyabiashara mbalimbali ili kuweza kutumia vipimo sahihi wakati wa biashara zao;
“Sisi kama Wakala wa Vipimo tunaadhimisha kwenye maeneo tofautitofauti tunayofanyia kazi kwa kuwafundisha wafanyabiashara jinsi ya kutumia vipimo sahihi sehemu mbalimbali”
Aidha Meneja huyo amesema kwa Mkoa wa Ilala wana sekta mbalimbali wanazifanya nao kazi hivyo kwa mwaka huu wameamua kuadhimisha siku ya Vipimo Duniani katika sekta ya biashara ya ujenzi;
“Kwa Mkoa wa Ilala tumeamua kuadhimisha kwenye maeneo tofauti yenye vifaa vya ujenzi kwasababu sisi Wakala wa Vipimo tuna sekta mbalimbali ambazo ni sekta ya Afya, Ujenzi, Kilimo, Biashara n.k hivyo kwa mwaka huu tumeamua kuchagua sekta ya Biashara kwenye upande wa ujenzi”
Kwa upande wake Afisa vipimo mkoa wa kivipimo Ilala, Denis Mtatilo amesema kwa Ofisi ya vipimo wanakuwa na ukaguzi wa mwaka, ukaguzi wa muda wowote, na ukaguzi wa kushtukiza ili kuhakikisha kwamba wanamlinda mlaji
Pia ameongeza kuwa Elimu wanayowapa wafanyabiashara ni namna bora ya ufungashaji ambao upo kwa mujibu wa Sheria ili kuweza kuwa na biashara shindani.
Naye Afisa Mauzo kutoka FM J Hardware LTD, Athman Kanyerere wanahitaji kumlinda mteja ambapo anapokwenda kununua bidhaa anakutana na ubora ambao anautarajia kwa kuhakikisha bidhaa inayokuja inafanana na size ambayo kiwandani imewapa
Pia ametoa wito kwa wafanyabiashara kujitahidi bidhaa wanayochukua kiwandani ifanane na uhalisia wa kile kipimo chenyewe ili kuepusha changamoto ndogondogo zinazojitokeza kwasababu mlaji wa mwisho anatakiwa atumie pesa yake kuendana na bidhaa yenyewe ilivyo.
More Stories
CPA.Makalla :CCM kutumia 4R za Rais Samia katika uchaguzi Serikali za Mitaa
CCM kutumia 4R za Samia Uchaguzi Serikali za Mitaa
Dkt. Mpango awasilisha salam za Rais Samia mazisha Baba yake mzazi, Gavana Tutuba