Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Ifikapo Mei 23 ya kila mwaka dunia uadhimisha siku ya kutokomeza ugonjwa wa fistula ambao uwapata wakina mama hususani wanaokutana na uchungu pingamizi wakati wa kujifungua.
Hivyo Tanzania kama ilivyo nchi nyingine kila mwaka uungana na nchi nyingine duniani katika kuadhimisha siku hiyo ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando mkoani Mwanza.
Akizungumza na timesmajira online Daktari Bingwa wa Afya ya uzazi, Mratibu wa Huduma za Fistula Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt.Elieza Chibwe, amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “zuia fistula,tokomeza fistula,wekeza kwenye huduma za afya ambapo mgeni rasmi wanatarajia atakuwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Dkt.Chibwe ameeleza kuwa katika maadhimisho hayo watatumia kujadili tatizo la ugonjwa huo ambapo jamii nyingi bado haina uelewa juu fistula zinawaficha wagonjwa ndani hususani maeneo ya vijijini wakiamini kuwa ni laana hivyo ametoa wito kwa jamii kutambua kuwa ugonjwa huo unatibika na matibabu yake ni bure.
“Jamii bado haina uelewa juu ya fistula tunapambana kuelimisha juu ya ugonjwa huu ambao unavisababishi vingi lakini wagonjwa wetu tunaowapata wengi ni waliopata uchungu pingamizi bila ya kuwa na msaada wa wataalamu wa afya wengi wao wanaishia kupata ugonjwa huu,”amesema Dkt.Chibwe.
Pia ameeleza kuwa kwa mujibu wa takwimu kila mwaka inasadikika kwamba wagonjwa wa fistula duniani kote wapo zaidi ya 100,000, lakini wengi wanapatikana katika nchi zinazoendelea Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo ni asilimia 95 ya idadi ya wagonjwa wote.
“Sisi kama nchi kila mwaka kuna wagonjwa wapya wapatao 2500-3000 lakini bahati mbaya wanaotibiwa kama 1,500 mpaka 2,000, kuna wagonjwa 1,000 kila mwaka hawapati matibabu ya fistula huku kwa mwaka Bugando tunapata wagonjwa wapatao 300-400 kwa mwaka na tunafanya upasuaji kwa wagonjwa zaidi ya 300 kwa mwaka,” amesema Dkt.Chibwe.
Hivyo ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa jamii kwenda Hospitali kwani ugonjwa huo unatibika na matibabu yake ni Bure.
Kwa upande wake mmoja wa wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Bugando Maria Elia ametoa wito kwa jamii kuhakikisha inapeleka wagonjwa wa fistula hospitali kwa ajili ya kupata matibabu kwani ugonjwa huo unatibika.
“Mimi nilipata fistula wakati najifungua,nikaletwa hapa Bugando nikapata matibabu na sasa nimepona na nitarudi nyumbani Serengeti ambapo nitawaeleza kuwa wanawapeleka hospitali watu wenye ugonjwa huu kwani unatibika na tiba yake ni kufanyiwa upasuaji na si kutumia dawa za miti shamba,” amesema Maria.
More Stories
Mwalimu adaiwa kumfanyia ukatili mwanafunziÂ
NAOT watakiwa kuendana na viwango vya ukaguzi
Rais Samia kuzindua mfuko wa kuendeleza kazi za wabunifu