Kampuni ya Halotel Tanzania imeendelea kuwahakikishia wateja ubora na kasi ya mtandao wake kwa kuwapa huduma zenye ubunifu na kuendelea kuboresha huduma za mawasiliano hapa nchini.
Wakati ikifanya jitihada hizo, Halotel pia imekuwa ikibuni bidhaa mpya zenye lengo la kuwazawadia wateja wake wanaotumia huduma za mtandao.
Mkurugenzi wa biashara cha Halotel, Bw. Abdallah Salum amesema: “Leo kampuni ina habari njema kwa wateja wetu: tunazindua kampeni mpya ya mtandao wa 4G. Kampeni hiyo inaitwa ‘Toboa na Halotel 4G.’
Kampeni hii itawapa fursa wateja kushiriki katika promosheni hii itakayoendeshwa kwa wiki 8 ambapo washindi watapata zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu na simu janja.
Ili kushiriki katika promosheni hii ya Toboa na Halotel 4G, wateja ambao wanatumia 3G wanaweza kubadili laini kwenda 4G bila gharama yoyote au mteja anaweza kusajili laini ya 4G na kuanza kutumia vifurushi vya intaneti kwa gharama nafuu na moja kwa moja atakuwa katika nafasi ya kuingia kwenye droo ya bahati na kuweza kuibuka mshindi.
Pia mteja anapaswa awe ameshatumia angalau 100MB ndani ya siku tatu kuanzia siku aliyoanza kutumia mtandao wa 4G. aliongeza Bw. Salum.
Kampuni itawazawadia washindi 10 kila siku, kila mmoja atapata fedha taslimu kiasi cha shilingi 100,000.
“Kila wiki washindi watatu (03) watazawadiwa simu janja ambapo mshindi wa kwanza atapata IPhone 13 pro max, mshindi wa pili atapata Samsung galaxy S22, na mshindi wa tatu atapata Samsung Galaxy A72,” Bw Salum alisema.
Kampuni imezindua kampeni hii kwa kuzingatia kwamba tayari mtandao wake wa 4G umeenea katika maeneo mengi ambapo kwa sasa ina vituo vipatavyo 1037 vinavyosambaza mtandao wa 4G, hivyo mtandao wa 4G umeongeza nguvu na ufikiaji wa maeneo mengi ya nchi.
Sababu zingine za kuanzisha kampeni hii ni kuwapa wateja uzoefu juu ya ubora wa 4G huku ikiwapitia zawadi mbalimbali, na hivyo kufanya huduma hiyo kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa sasa mtandao wa 4G umewafikia asilimia 45 ya Watanzania.
“Hii ni kutokana na kukua kwa huduma za kidijitali hapa Tanzania na kuongezeka kwa uhitaji katika soko, na hivyo uwekezaji mkubwa wa kampuni umeelekezwa kwenye miundombinu katika juhudi za kuongeza vituo vya usambazaji mtandao wa 4G,” amesema Bw. Salum.
Ameongeza kuwa katika maeneo ambayo yana mtandao wa 2G kampuni itaboresha na kuwa 3G na maeneo yenye 3G watapata 4G.
Halotel itawekeza zaidi kuongeza ubora wa mtandao Kwa sababu Watanzania milioni 29.8, au karibu nusu ya Watanzania wanatumia huduma za intaneti, tafiti mpya inaonesha kuwa Halotel ina mtandao wenye kasi zaidi kuliko mitandao yote hapa nchini.
Kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita kampuni imekuwa ikijielekeza katika mikakati ya kupanua wigo wa mtandao wake hapa Tanzania.
Kwa kuzingatia kuwa asilimia 30 ya wateja wake wanatumia mtandao wa intaneti, kampuni inapanga kuongeza idadi hiyo kufikia asilimia 40 ifikapo mwisho wa mwaka huu.
Halotel tayari imeanza kuzindua kizazi cha nne cha huduma za mtandao wa 4G katika maeneo mengi ya nchi.
More Stories
Bumbuli kutekeleza miradi kwa kuangalia vipaumbele
Makalla:Kupanga fujo ni dalili za kushindwa uchaguzi
Tanzania yapanda viwango Utawala wa Sheria Duniani