Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Katika kupambana na vifo vya uzazi kwa kina mama Halmashauri ya Jiji la Mwanza linachukua hatua mbalimbali kuhakikisha vifo hivyo vinapungua au kumalizika kabisa.
Hayo yameelezwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Dkt. Sebastian Pima,wakati akizungumza na timesmajira online ofisini kwake jijini Mwanza.
Ambapo ameeleza kuwa ndani ya halmashauri hiyo wanayo Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando ambayo kimsingi inapokea wagonjwa kutoka mikoa ya Kandaya Ziwa,kwa sababu hiyo wanapata wagonjwa wengi ambao wanakuwa kwenye hali ambayo pengine inakuwa ngumu kuwaokoa.Dkt.
Pima amesema, wamechukua hatua mbalimbali kuhakikisha vifo vya kina mama vinavyotokana na uzazi katika Jiji lao vinaweza kupungua.
Ameeleza kuwa,wamefanya tathimini wamebaini kwamba vifo vingi vya uzazi vinatokana na kutoka damu aidha kabla,wakati au baada ya kujifungua.
Hivyo hatua walizo weza kuchukua katika kukabiliana na changamoto hiyo ni wameweza kuimarisha huduma zao za kliniki kwa kuhakikisha kwamba wanawapatia watoa huduma wao mafunzo ambayo yatawezesha kutoa huduma bora.
Pia ameeleza kuwa ili waweze kutoa huduma bora kwenye kliniki lazima mteja aje kwaio wamepeleka ujumbe kwenye jamii ambapo wanapita kwenye mitaa na kata zao wanatoa elimu ya umuhimu wa kina mama wajawazito kuhudhuria kliniki.
Ambapo wamekuwa wakiwahamasisha kuwa wahudhirie kliniki mara tu wanapogundua kwamba ni mjamzito ili basi waweze kupangiwa mpango mzuri wa kuhudhuria kliniki na kuweza kubaini vidokezo vya hatari mapema wakati wa kujifungua ili akiona dalili yoyote ya hatari basi aweze kuchukua hatua stahiki.
“Kupitia hivyo sisi tunaamini mnyororo huu wa huduma kwa ujumla wake ukiimarika kwa maana mafunzo kwa watoa huduma,vifaa, hupatikanaji wa damu na vitu vingine kama hivyo kwa ujumla wake sasa utasaidia utoaji wa huduma kufikia kiwango kinachokubalika na kuweza kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi,”ameeleza Dkt.Pima.
Aidha ameeleza kuwa wanaendelea kupambana navyo kwa kasi kubwa lakini bado vinawasumbua,wanashukuru huduma nyingi za kibingwa zinazidi kuongezeka nchini hapa na katika maeneo yao wanayafanya kazi,wanaamini kupitia hivyo wananchi watapata faida na lengo la kuona Tanzania yenye rasilimali ya watu linaweza likafikiwa.
More Stories
Makalla:Kupanga fujo ni dalili za kushindwa uchaguzi
Tanzania yapanda viwango Utawala wa Sheria Duniani
Rais Samia apeleka neema Tabora