November 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wadau wa maendeleo wapanga mikakati ya kuboresha sekta ya uvuvi

Na mwandishi wetu,timesmajira,Dar es Salaam 

Shirika la  Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kupitia mradi wake wa FISH4ACP limefanya mkutano wa pili wa Kikosi Kazi cha Taifa cha kukuza mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma.

Mkutano huo umefanyika mkoani Kigoma kwa lengo la kujadili na kupitisha mkakati wa uboreshaji wa mradi wa  FISH4ACP na mpango wa utekelezaji wa mradi huo kama hatua ya kutatua  changamoto zinazoikabili sekta ya uvuvi kupitia mradi huo  wa miaka mitano unaotekelezwa na FAO ambao umeanza mwezi Septemba 2020.

Hayo yameelezwa na Afisa Mtaalamu Mnyororo wa Thamani wa Uvivu na Ufugaji Viumbe Maji, kutoka FAO nchini Tanzania anayesimamia mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma nchini , Hashim Muumin amesema mradi huo unatekelezwa katika Nchi 12 za Afrika  ikiwemo  Tanzania .

“Mradi huu umekuja na mikakati minne  ambayo  ni kusaidia wachakataji wa  mazao ya uvuvi wa Ziwa Tanganyika yakiwemo dagaa na migebuka, kupata masoko katika kanda hii na nje ya kanda na kutokana na utafiti tumebaini suala la  mitaji kutoka katika taasisi za kifedha itakayowasaidia kuboresha shughuli zao na sisi tutawapatia mafunzo,”amesema Mratibu huyo.

Aidha  Hashim amebainisha kuwa ujio wa mrad huo utasaidia kuimarisha na kujenga mazingira rafiki kwa wanawake ili kufanya shughuli zao katika nyanja ya uchakataji, wafanyabiashara na usafirishaji ili  kuongeza kipato binafsi na pato la Taifa.

Naye Mteknolojia Mwandamizi wa samaki kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (sekta ya uvuvi),Masui Munda amesema kwamba ujio wa mradio huo utachnagia kwa kiasi kikubwa kuinua sekta ya uvuvi kama ilivyo azima ya Serikali  kwani uvuvi huchagiza ukuaji wa uchumi.

“ Kwa upande wa wizara sasa hivi dagaa ni zao la kimkakati kwahiyo inatumia fursa zilizopo kuinua mnyororo wa thamani wa mazao haya yanachakatwa kwa ufanisi, ubora na usalama kwa walaji ndani ya nchi na nje ya nchi kama tulivyo na masoko Canada, Austrelia na Marekani lakini bado tunataka uongeza wigo,”amesema Mteknolojia huyo.

Vile vile mchakati kutoka mwalo wa Kibirizi mkoani Kigoma Betina Tito na kiongozi wa vyama vya Uvuvi mkoa wa Kigoma, Francis John walishukuru FAO na serikali kwa kuwapatia elimu ya uvuvi salama utakaosaidi kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi.