November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kilimo Cha zao la mchikichi kuokoa shilingi Bilioni 470

Na Ashura Jumapili, TimesMajira Online, kagera

WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ,amesema serikali imehamasisha kilimo cha zao la mchikichi lengo likiwa ni kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 470 zinazotumika kila mwaka kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi.

Waziri Majaliwa ,ametoa kauli hiyo leo mjini Bukoba mkoani kagera wakati akiongea na wakuu wa wilaya,wakurugenzi,maofisa ushirika ,wadau wa kahawa na watendaji wa serikali ya mkoa huo.

Alisema wakulima wamepokea vizuri mkakati wa serikali wa kuendelea kulima zao hilo na kudai kuwa lengo ni kuongeza mafuta nchini yanayozalishwa na wazawa badala ya kutumia ghama kubwa kila mwaka kuagiza mafuta nje ya nchi.

Pia amewaagiza viongozi wote wa serikali kuhakikisha kila mkoa unalima kilimo cha alizeti ii kuweza kupata mafuta ya kutosha.

Alisema mwanzo serikali ilianza na mazao matano ya kimkakati ambayo ni Pamba,Kahawa,Chai,tumbaku na korosho

.“Tumepanua wigo wa mazao tumeongeza mazao yanayolimwa na watu wengi kwenye maeneo yao.”alisema Waziri Mkuu.

Alisema wamehamasisha wakulima kulima kilimo cha mchikichi,wamefufua zao la mkonge sanjari na kuunda bodi yake.

Alisema zabibu ndio zao bora linalotoka Tanzania kwa nchi za Afrika na linavunwa mara mbili kwa mwaka nalo limeingizwa kwenye mfumo.

Alisema wanaendelea kuyasimamia mazao hayo kuanzia kilimo ,pembejeo na masoko.

“Tunataka wananchi wapate faida ya kilimo wanacholima katika mazao hayo ya kimkakati ili kilimo kiwe na tija”alisema.

Viongozi mbalimbali waliohudhuria mkutano huo akiwemo Meya wa Manispaa ya Bukoba Gypson Godson kwa kwanza kulia