November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mutafungwa: Naridhishwa na hatua za kupuguza ajali barabarani

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mkuu wa kikosi cha poilisi cha usalama barabarani SACP Wilbroad Mutafungwa ameeleza kulizishwa  na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na madereva wa mabasi na wenye maroli juu ya  utii sheria bila shuruti  juu ya kuhakikisha ajali za barabarani hazitokei .

Akiongea na waandishi wa habari mjini Kahama juzi akiwa kwenye oparesheni ya kuthibiti makosa hatarishi ya usalama barabarani aliyoanza toka  Gairo hadi  mikoa ya kada ya kati hadi ya kanda ya ziwa alisema amelizishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na wenye magari na madereva juu ya kuhakikisha ajari hazitokei.

Mutafungwa alisema oparesheni hiyo ya kukamata magari yanayovunja sheria na yanayobainika kuwa mabovu  aliianza mei 11 katika barabara kuu ya rami kutoka Gairo kwenda mikoa ya kanda ya kati na ya ziwa  ambapo ameeleza kulizishwa na hatua za madereva za utii wa sheria  za usalama barabarani.

Alisema kwenye oparesheni hiyo toka tarehe hiyo amefanya ukaguzi wa mabasi ya abiria zaidi ya 173 kati ya hayo 87 yalifaata sheria na 47 yalikamatwa na  kupigwa faini kwa sababu mbalimbali za kutotii sheria za usalama barabarani na madereva 9  walipewa onyo kali na mabasi 8 yalibainika na kosa la mwendo kasi.

Mutafungwa alisema katika ukaguzi huo mabasi 15 yalibainika kuwa na ubovu mbalimbali  na kuyachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuyasitishia safari hadi yafanyiwe matengenezo  na pia alieleza  kumekuwepo na  mchezo mchafu unaofanywa na mabasi ya kuharibu sistimu  ya kuonekana kwenye mfumo kudhibiti mwendo.

Kwa upande wa maroli ya mzingo alisema ametoa semina ya siku moja kwa madereva  67  katika kituo cha Misigiri  kuhusu  utii wa sheria  za usalama barabarani  ambapo amewataka  wale wote wanaoendesha vyombo vya moto  kutii alama za barabarani na wasitumie vileo  na kuchana  mwendo kasi na kuyapita magari mengine  bila kuwa makini.

Mutafungwa alisema lengo la oparesheni hiyo ni kuhakikisha ajari za barabarani zinapungua  ambapo ametoa wito kwa madereva na wenye magari , waendesha bodaboda kufaata sheria wanapoendesha vyombo vya moto kwa sababu anatamani siku moja pasiwe na askari barabarani  bali sheria peke yake zifanye kazi.

Mkuu wa kikosi cha polisi cha usalama barabarani , SACP. Willbord Mutafungwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mjini Kahama ,hawapo kwenye picha alipokuwa akieleza mafanikio ya oparesheni yake ya kudhibiti makosa hatarishi ya usalama barabarani ili kupunguza ajari za magari , Picha na Patrick Mabula.
Mkuu wa kikosi cha polisi cha usalama barabarani Willbord Mutafungwa akitoa maelekezo ya kazi kwa askari wa usalama barabarani wa wilaya ya Kahama alipokuwa kwenye opareshini ya kudhibiti makosa hatarishi ya usalama barabarani kwa lengo la kuzuia ajari za magari,Picha na Patrick Mabula