Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Miili ya Askari wawili wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,walioipata ajali juzi Aprili 27 mwaka huu Mkoani Geita imeagwa na kusafirishwa kuelekeza katika mikoa ya Singida na Mara kwa ajili ya kuhifadhiwa katika nyumba zao za milele.
Ambapo ajali hiyo imehusisha watu wanne waliopteza maisha wakiwemo Polisi hao wawili na watuhumiwa wawili huku watu wengine wanne wakiwa majeruhiwa baada ya kupata ajali eneo la kijiji cha Ibanda barabara ya Geita kuelekea Sengerema iliyohusisha gari la Polisi na lori iliotokea majira ya saa 10.30 Aprili 27 mwaka huu.
Waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Askari G.4467 D/CPL Mussa Mahamba na H.5702 D/C Faraji Bayu pamoja na watuhumiwa wawili wa makosa ya vitendo vya ugaidi na mauaji ambao ni Twaha Saidi na Tesha Luiza waliokuwa wakisafirishwa kutoka mkoani Geita kusikiliza shauri lao mahakamani kwenda gereza la Butimba mkoani Mwanza na wakiwa njiani ndipo walipokutwa na mauti.
Majeruhiwa wa ajali hiyo ni PF.23158 A/INSP Baraka Apila na F.8361 D/SGT Berison Sanga wote wakiwa Askari wa Polisi Mkoa wa Mwanza.
Wengine ni Maronja Katemi ambaye ni dereva wa gari ya Kampuni ya Nyanza Bottling mkazi wa Igoma Mwanza pamoja na Paulo Charles Mfanyakazi kwenye gari la Kampuni ya Nyanza Bottling.
Akizungumza wakati wa zoezi la utoaji heshima za mwisho kwa Marehemu hao lililofanyika Katika uwanja wa FFU Polisi Mabatini Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel amesema imempendeza Mungu kuwaondoa katika umri huo vijana hao ambao ni amana na wapambanaji wa taifa ambao wamefia wakiwa wakitimiza majukumu yao.
“Tunamshukuru Mungu kwa maisha yao hapa duniani,tunaweza kujiuliza kwanini muda huu lakini njia za Mungu hazichunguziki,kuishi miaka mingi siyo kuwa ni baraka pengine Mungu anawaacha ili watubu hivyo wazee wasiwe na kiburi ila ni rehema za Mungu na imempendeza Mungu vijana hao kuondoka katika umri huo wa ujana,” amesema Mhandisi Gabriel.
Kwa upande wake kaka wa Askari G.4467 D/CPL Mussa Mahamba,Mwita Mahamba amesema, wanamshuku Mungu kwa sababu ametenda kazi yake,Jeshi la Polisi, serikali na wananchi kwa ujumla,ambapo jambo hilo limewashtua lakini hawana jinsi.
“Unapoona vifo,magonjwa na ajali basi ni kampeni ya Mungu kutafuta watu wake ,sote tujiandae na tuwe tayari mwili wa marehemu mdogo wangu tunausafirisha kwenda Rorya mkoani Mara,” amesema.
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke,amesema Jeshi la Polisi wanafanya kazi kubwa ambayo inapaswa kuwaombea kila wakati huku akiwataka wananchi na waumini wa dini zote kumrudia Mungu kwani siku ikifika hakuna anayeweza kukimbia na kifo akichagui.
More Stories
Makalla:Kupanga fujo ni dalili za kushindwa uchaguzi
Tanzania yapanda viwango Utawala wa Sheria Duniani
Rais Samia apeleka neema Tabora