Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amesema Kudorora kwa miradi kwenye Halmashauri ya wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kunakwaza wananchi na Ofisi ya Rais -TAMISEMI.
Waziri Bashungwa ameeleza hayo baada ya Mbunge wa Mvomero Jonas Van Zeeland kueleza hali ya ubadhilifu na upotefu wa fedha iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ambayo ilibainiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI na kutolewa maelekezo japo mpaka sasa maelekezo hayo hayajatekelezwa.
“Nilifanya ziara hapo Machi 10 mwaka huu nikatoa maagizo. Kabla sijazinguliwa kuna watu nitazinguana nao. Sitakubali kumkwaza mheshimiwa Rais na Watanzania.” amesema Waziri Bashungwa
Aidha, Waziri Bashungwa amezitaka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuongeza kasi katika kutoa huduma bora na kukamilisha miradi kwa wakati na kwa uaminifu na kuondokana na Ubadhilifu.
Ikumbukwe kuwa, tarehe 10 Machi, 2022 Waziri Bashungwa alibaini upotevu wa fedha na matumizi yasiyosahihi ya kiasi cha shilingi milioni 231.84 katika ujenzi wa shule ya Sekondari ya kumbukumbu ya Sokoine kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la chakula, miundombinu ya jiko na bweni na kuagiza kuwachukukiwa hatua za kiutumishi wakuu wa Idara wote waliohusika na ukiukwaji wa taratibu za Manunuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.
More Stories
Mwalimu adaiwa kumfanyia ukatili mwanafunzi
NAOT watakiwa kuendana na viwango vya ukaguzi
Rais Samia kuzindua mfuko wa kuendeleza kazi za wabunifu