Na Nasra Bakari, TimesMajira Online
WIZARA ya Maliasili na Utalii imeombwa kuwarudishia mifugo na kuwalipa fidia wafugaji ambao walishinda kesi zao mahakamani.
Akizungumza bungeni jana mkoani Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mary Masanja alisema mpaka sasa hawajapata orodha kamili ya wafugaji ambao wanalalamika hawajarejeshewa mifugo yao.
“Orodha ipo wizarani na waziri anayo kwanini Naibu Waziri unakwepa kuwalipa hao wafugaji wanyonge ambao walishinda kesi yao mahakamani na kutudanganya hapa orodha hiyo hauna,” alihoji Mbunge huyo.
Naibu Waziri huyo alijibu, kama nilivyotangulia kusema mwanzoni katika swali la msingi kwamba kesi inapopelekwa mahakamani sisi kama wizara hatuhusiki tunapeleka vielelezo tu.
Alisema, na kesi inabaki kuwa chini ya hakimu na DPP na wao wanabaki kuwa mashahidi kwamba mifugo iliyokamatwa ni hii na baada ya hapo Hakimu ndiyo anatoa hukumu .
“Endapo kama kuna mfugaji ambaye ana kesi ya kutudai sisi wizara ya malisili basi aje wizarani tutakaa pamoja kuichambua hiyo kesi na tutaweza kuichambua sisi kama Serikali,” alisema Masanja.
More Stories
Bei za mafuta Novemba 2024,zaendelea Kushuka
TARURA yaomba Mkandarasi aitwe
Ilemela yakusanya bilioni 3.7.robo ya kwanza