Na David John,TimesMajiraoniline
MWENYEKITI wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Limited nchini Tanzania Dkt. Seleman Majige Ametoa Tuzo kwa wasambazaji na watoa huduma ya mafuta kwenye vituo vya mafuta huku Puma Energy wakija na mkakati wa kuaza kuuza Nishati ya Gesi ya Majumbani kupitia vituo vyao vyote vya Mafuta hivi karibuni.
Dkt..Majige Amesema kuwa kwakuwa kampuni ya Mafuta ya Puma Energy ndio namba moja na yenye huduma bora hapa nchini hivyo hata kwenye uuzaji na usambazaji wa Nishati ya Gesi watakuwa namba moja Kama ilivyo kawaida yao.
Mwenyekiti huyo wa Bodi ameyasema hayo wakati wa sherehe ya kutoa tuzo hizo ambao umefanyika katika ukumbi wa Golden Jubilee Mkoani Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mwakilishi kutoka Hazina, wafanyabiashara pamoja na wasambaji na watoa huduma kote nchini.
“Nawapongeza wote mliopata tuzo hizi na kwakweli tunajivunia kwa huduma bora ambazo mnazifanya na niwaombe mkaendelee kuitangaza, na kuilinda Puma Energy limited ili iendelee kuwa kampuni namba moja kwa ubora. “amesema Dkt Majige
Nakuongeza kuwa “Hivi karibuni tunakwenda Kuaza kufanya huduma ya Biashara ya usambazaji wa nishati ya Gesi ya majumbani kwani tayari Bodi imeshakaa na kupitisha hilo hivyo matarajio yangu nikuona tunaendelea kuwa namba moja kwa ubora wa huduma zetu hivyo nawapongeza nyote kwa kazi nzuri mnayofanya. “amesisitiza Mwenyekiti Dkt Majige
Akizungumzia Kampuni hiyo amesema kuwa wameendelea kuwa namba moja kwani kila kituo ambacho utakwenda utakuta huduma hiyo ya mafuta na hivi sasa wameongeza vituo kutoka 52 vya awali nakufikia vituo 80 lakini lengo nikuona hadi kufikia mwaka 2025 wanakuwa na vituo 150 na sio 100.
“Niombe Menejimenti ya Kampuni hii ya Puma kwamba hadi kufikia mwaka 2025 muwe mmeongeza vituo hadi kufikia 150 na sio 100 kama mlivyokuwa mmepanga mimi naamini tunaouwezo wa kufikia vituo 150 hivyo tujielekeze huko kwani uwezo upo na muhakikishe vituo hivyo vinafikia. “Amesema Dkt. Majige
Dkt Majige amewaeleza wadau hao na kuwakumbusha Kuwa Puma ni kampuni kubwa hivyo waendelee kuilinda na kuhakikisha mafuta yanakuwa salama lakini pia ameitaka menejimenti kuweka mkakati wa kuazisha vituo vijijini ili kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi wengi zaidi.
Amemaliza kwa kuendelea kuwakumbusha watoa huduma kutumia maneno mazuri kwa wateja kwani hiyo ndio silaha ya Puma energy kuwa namba Moja na kwakufanya hivyo kutawafanya wateja kufurahia huduma zao Kama ilivyokawaida.
Awali wakati akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Limited Tanzania Dominic Dhanah Amesema Kampuni hiyo ndio inayoongoza nchini na inashika namba moja kwa ubora.
Amesema kuwa namba moja ni kazi kubwa sana lakini wataendelea kuwekeza na kwamba hadi kufikia sasa Puma inavituo 80 kutoka vituo 52 vilivyokuwepo hapo mwanzo na lengo nikufikisha vituo 100 kufikia mwaka 2025.
“Ndugu Mgeni rasmi kampuni imeendelea kuwa bunifu na tumeongeza huduma nyingine ya vilainishi vya kwenye magari na mapema mwaka huu tunatarajia kuzindua nishati ya gesi ya majumbani ambayo itakuwa inapatikana kwenye vituo vyetu vyote na hakuna shaka kwamba itapokelewa vizuri. “Amesema Dhanah
Pia amewapongeza watoa huduma wote wa Puma energy na kwamba wao ndio chachu ya mafanikio ya kampuni hiyo huku akiwataka kuendelea kuendelea kufanya vizuri zaidi na katika tuzo hizo kituo cha mafuta kutoka Arusha cetral station kimefanikiwa kuwa mshindi wa jumla wa uuzaji wa mafuta na hiyo ni mwaka wa pili mfululizo.
Katika tuzo hizo washiriki walifanikiwa kupata tuzo ya vikombe na pesa taslimu sh.laki 2.5 kama motisha na kuwapa hamasa ya kuendelea kufanya vizuri zaidi.
More Stories
TARURA Kilimanjaro yatimiza ahadi ya Rais Samia
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria
Wananchi wakubali yaishe Bangi kubaki historia Tarime