Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Chama cha waajiri nchini (ATE) kimezindua awamu ya 8 ya Programu ya Mafunzo ya Mwanamke Kiongozi ambapo jumla ya Wanawake 73 Kutoka katika makampuni mbalimbali nchini watafanya mafunzo hayo yenye mpango wa kuongeza idadi ya wanawake wanaoshika nafasi za juu katika bodi za maamuzi ikiwa ni katika jitihada za kuwainua wake na masuala ya uongozi nchini.
Akizungumza jijini Dar e Salaam wakati wa Ufunguzi wa Awamu ya 8 wa mafunzo hayo ambayo yameanza kutolewa tangu mwaka 2006 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Nchini (ATE), Suzanne Ndomba- Doran amebainisha kuwa mafunzo hayo hadi sasa yameshawafikia wanawake 208 ambapo yamekuwa yakitolewa kwa kushirikiana na Shirikisho la Waajiri la Norway (NHO) ikiwa ni kusaidia kuongeza idadi ya wanawake viongozi katika bodi za maamuzi kama mkakati wa kuwainua wanawake ambao wengi wao wamekuwa nyuma katika Nafasi za uongozi.
Mbali na hayo Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kwa mwaka huu mafunzo hayo yamekua kwa kasi ambapo wamezindua Programu ya wanawake na baadaye kwa wabunge wanawake na Wajumbe wa Baraza la wawakilishi Zanzibar.
“Mpango huu uendelea kukua kwa kasi ambapo sasa mafunzo haya yameanza kutolewa hadi kwa viongozi wa Umma na hadi sasa tayari tumezindua Programu ya Mwanamke Kiongozi kwa kwa Wabunge Wanawake na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, hii ina maana tutakuwa na wanawake wengi zaidi waliofuzu mafunzo haya katika siku za usoni.”
Suzanne alisema kuwa wataendelea kushirikiana na wadau wengine katika utetezi wa sera unaolenga kuongeza idadi ya wanawake katika nafasi za juu za uongozi na katika bodi mbalimbali pamoja na kushirikiana na makampuni katika kuhakikisha kuwa sera zao zinawiana sawa.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa kampuni ya Madini ya GGM Simon Shayo amebainisha kuwa bado idadi ya wanawake katika ngazi ya maamuzi haitoshelezi hivyo ni vyema jitihada za kuwapa mafunzo zikaungwa mkono ili kuongeza idadi ya Wanawake katika bodi za Mkampuni hapa nchini Tanzania huku akitaka kutungwa kwa sheria ya ajira itakayowalinda katika bodi za maamuzi.
Naye mmoja wanawake wanaoshiriki mafunzo hayo Hellen Mallya alisema programu hiyo itarejesha ujasiri wa kina kwa wanawake wengi katika kuwania nafasi za juu katika uongozi wa makampuni hali ambayo awali haikuwepo.
More Stories
Chande azindua misheni ya uangalizi uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika
CPA.Makalla :CCM kutumia 4R za Rais Samia katika uchaguzi Serikali za Mitaa
CCM kutumia 4R za Samia Uchaguzi Serikali za Mitaa