Na Nasra Bakari, TimesMajira Online
WANANCHI wa Mtaa wa Mwananyamala Kisiwani wameitaka serikali kupitia manispaa ya kinondoni kuwaondolea kero ya matakataka yaliyojazana katika makazi ya watu na kupelekea kuleta magojwa ya mlipuko.
Wakizungumza jana jijini Dar es Salaam Katika ofisi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo,wamesema kero hiyo inawafanya kutokujishughulisha na biashara zao ndogondogo hususani zile za vyakula kwani mazingira si rafiki kwa afya.
Wananchi hao walisema matakataka hayo utolewa katika nyumba za watu na kukusanywa sehemu moja ambapo gari linapochelewa kuja kuyatoa usababisha vijidudu kusambaa ikiwa kuna Watotowadogo wanacheza.
“Kila mwananchi anatozwa shilingi 1000 ya matakataka lakini hayaondolewi kwa wakati na kusababisha baadhi yao kuyatoa majumbani mwao na kuyaweka barabarani kiasi kinachowafanya wafanayabiashara kusimama kwa muda usiojulikana,”alisema na kuongeza
“Gari la ubebaji takataka halipiti kwa wakati sahihi wakati pesa zao
zinakusanywa wanakusanyakila mwezi,” alisema Maua Fugo mmoja wa wafanyabiashara wa makazi hayo.
Alisema, hali hiyo inawafanya wao kusimamisha biashara zao kwa sababu takataka hizo zilizopo barabarani zinatoa wadudu na huenda wakasababisha magojwa ya mlipuko.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa huo, Ismaili Mohammedy alisema, ni kweli kuna changamoto ya uzoaji wa takataka ulijitokeza hivi punde hivyo tunawaomba wananchi wavumilie kwa muda wao kama serikali watalitatua.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa