Na Esther Macha,Timemajira Online, Mbeya
WENYEVITI wa vijiji na vitongoji mkoani Mbeya wameagizwa kuwa mabalozi na kutoa elimu ya umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji kwa wananchi kwa kuhamasisha upandaji wa miti itakayosaidia kutunza mazingira.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya maji na usafi na mazingira Jijini Mbeya (UWSA), Edina Mwaigomole amesema leo wakati wa uzinduzi  wa wiki ya maji ambapo Mamlaka ya maji  hiyo kwa kushirikiana kampuni ya Bia (TBL ) ilipanda miti 500 na kuwa mpaka kilele cha wiki ya maji kuisha watakuwa wamepanda miti 1500 kwenye vyanzo  vitatu tofauti   vya maji  vilivyopo Mkoani Mbeya.
“Nawaomba sana tuwe mabalozi wa kuwaambia wananchi wapande miti katika maeneo yao wanayoishi ,kwenye mito ,madibwi , lakini pia hyata miti iliyopandwa mwaka jana iendelee kutuzwa na hata hii miti 500 iliyopandwa leo itunzwe na isiwe kwamba baada ya kupandwa leo hii miti hakuna ufuatiliaji kuwa kujua maendeleo ya ukuaji wake “amesema Mwaigomole.
Hata hivyo amesema kuwa itakuwa ni bora zaidi kuelimisha wananchi mpaka ngazi ya kaya pamoja na kushiriki katika maeneo yao katika kupanda miti .
Amesema suala la kutunza mazingira ni muhimu sana na kuwa hakuna asiyejua umuhimu wa maji katika maisha ya kila na masuala mazima ya uchumi na katika viwanda vinavyotumia maji ni viwanda vichache sana ambavyo hatumii maji lakini viwanda vingi vinatumia maji .
“Kwa maana wiki hili la wiki hili la maji linatukumbusha kuwa majukumu yetu katika kutunza mazingira ili yaendelee kuwepo kwa kizazi hiki na kinachokuja sisi tumezaliwa tumeyakuta maji ni vema na sisi tukaacha maji wale wanaotufuata wakute maji yapo waendeleze kizazi kilichopo”alisema
Kwa upande wake Mwangalizi wa mazingira wa Kampuni ya bia (TBL ),Mhandisi ,Charles Aloyce amesema kuwa kampuni ya TBL ni wadau wakubwa wa utumiaji wa maji huwa wanapenda kujumuika na mamlaka ya maji kupanda miti pamoja na kusafisha vyanzo vya maji ili viweze kuwa mazingira mazuri ya kusambaza maji kwa jamii.
Kwa mujibu wa Kaimu mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na mazingira ,Saimon Bukuku amesema kuwa wanakusudia kupanda miti 1500 katika vyanzo vitatu vya maji ambavyo ni Mwashali , Itangano , Ilunga na kwamba kuna wakati huwa wanapanda miti lakini kuna watu hupita na kung’oa lakini kufuatia uharibifu huo wameanza kutoa elimu pamoja na kuweka walinzi wa kampuni kwenye vyanzo vyote ili vyanzo viwe salama pamoja na kuwa maji ya kutosha.
Naye Kaimu Meneja wa wakala wa maji vijijini (RUWASA) Emile Mpasi amesema kuwa kupitia wiki hilo la maji wataendelea kutambulisha miradi mbali mbali inayotekelezwa na serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha kuwa wanamtua ndoo kichwani mwanamke .
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â