Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo Albert Msando kwa kushirikiana na Taasisi ya NGAIZA FOUNDATION wanataraji kuendesha zoezi la utatuzi na usuluhishi wa Migogoro mbalimbali Wilayani humo ili kuiwezesha Serikali kupunguza changamoto hiyo.
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Eizabeth Ngaiza amesema zoezi hilo litakuwa endelevu na miongoni mwa Mambo yatakayoshughulikiwa ni pamoja na Migogoro ya Ardhi, Mirathi, usuluhishi wa Migogoro ya ndoa pamoja na suala la matunzo ya mtoto.
Aidha Ngaiza amesema Taasisi hiyo itatoa huduma hiyo bila malipo Chini ya Wataalamu wa masuala ya kisheria na utatuzi waliojitoa kuhakikisha kila Mwananchi atakaewasilisha kero na changamoto yake anasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi Jambo lake.
Hata hivyo Ngaiza amesema tayari Taasisi yake imefanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando ambae amepokea kwa mikono miwili Jambo hilo na ameahidi kushirikiana kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
Pamoja na hayo amesema anaamini kupitia Usuluhishi itasaidia kupunguza mlundikano wa kesi zisizo na ulazima Mahakamani kwakuwa kipaombele Cha Taasisi hiyo ni upatanishi na pale inaposhindikana ndipo kesi zifikishwe ngazi ya Mahakama.
Sanjari na hayo ametoa wito kwa Wananchi Wenye Migogoro kujitokeza kwa wingi kuwasilisha mashauri yao.
More Stories
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar
CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo
Walimu elimu ya lazima watatakiwa kuwa wabobezi kwenye masomo wanayofundisha