Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Mrisho Kikwete na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la AGRA ametembelea na kuona shughuli za uzalishaji  na usambazaji wa nafaka mbali mbali  wa Kampuni ya Raphael Group iliyopo eneo la Uyole Jijini Mbeya na kuwataka kuongeza tija  na kuwepo kwa chakula cha ziada .
Kikwete amesema hayo jana wakati alipotembelea kampuni hiyo kwa lengo la kuona shughuli za uzalishaji za kampuni hiyo ambazo ni ukoboaji mpunga,uandaaji na ufungashaji, kilimo cha mkataba na wakulima , ukamuaji wa mafuta ya alizeti ununuzi wa uchataji mahindi ununuzi na uuzaji wa mchele , uuzaji wa maharage,uuzaji mtama na Soya pamoja na uzalishaji mwingine.
Aidha Kikwete amesema katika kuona wakulima kuzalisha mazao  ya kimkakati wanatoa mafunzo kwa wataalamu kupitia Agra katika shahada ya uzamili na nyinginezo lengo ni kuona wakulima wadogo na kwa  Tanzania wamezalisha wataalam 42 wataokaosaidia katika Sekta ya Kilimo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Raphael Group ,Raphael Ndelwa amesema kuwa baada ya kujiirimarisha vyema katika shughuli kampuni hiyo iliona fursa za kufanya kazi na wakulima wadogo wadogo ili kujihakikishia upatikanaji wa malighafi wa mazao zinazotakiwa kwa wingi , ubora kwa wakati muafaka.
Ndelwa amesema kuwa kwa madhumuni hayo kampuni hiyo ilianza kufanya kazi na wakulima wa mazao moja kwa moja mwaka 2010 ambapo kipindi chote cha nyuma ili kutegemea ununuzi wa mazao kutoka kwa wanunuzi wa kati .
Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa mpaka sasa kampuni hiyo inafanya kazi kwa mfumo wa kilimo cha mkataba na wakulima zaidi ya 15,000 ambao wamejiajiri katika kilimo ambapo wakulima wa mpunga ni 10,000 na wakulima wa Maharage zaidi ya 5,800.
Katika ziara hiyo, Rais mstaafu Kikwete amefuatana na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde pamoja na viongozi wa shirika la AGRA na Britten.
More Stories
Rais Samia kuzindua mfuko wa kuendeleza kazi za wabunifu
Makalla ampongeza Lissu kukiri CHADEMA haina wagombea Serikali za Mitaa
Chande azindua misheni ya uangalizi uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika