November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Miwili wa Dkt.Mwele kuzikwa Jumatatu Dodoma

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

MWILI wa marehemu aliyekuwa Mkurugenzi wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele katika Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt.Mwele Malecela aliyefariki dunia siku ya Alhamisi unatarajiwa kuzikwa Mvumi mkoani Dodoma Machi 21, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa fupi ya ratiba ya mazishi msemaji WA familia, Samweli Malecela alisema kuwa mwili wa marehemu utawasili saa tano usiku na kupokelewa na ndugu na jamaa.

“Mwili wa marehemu utawasili Dar es Salaam siku ya Ijumaa saa 5 usiku uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na utapokelewa na ndugu, jamaa na marafiki.

“Baada ya mapokeizi msafara wa mapokezi utaelekea moja kwa moja s
Sea View nyumbani kwa Mzee Dkt. John Samweli Malecela ambapo utalala hapo” alisema.

Aidha Samweli alisema siku ya Jumamosi asubuhi kutakuwa na sala fupi itakayofanyika nyumbani na baada ya sala mwili utaelekea Kanisa la Mtakatifu Albano ambapo saa 3 asubuhi misa itafanyika.

Samweli aliongeza kuwa baada ya kumalizika kwa ibada mwili utaelekea Karimjee kwa ajili ya kutoa heshima za pamoja na Salam mbalimbali za rambirambi.

Alisema kuwa shughuli ya kuaga unatarajiwa kumalizika saa 10 jioni na kisha mwili kuelekea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kwa ajili ya safari ya kuelekea Dodoma kwa mazishi.

Mbali na hayo kaka wa marehemu alisema kuwa siku ya Jumapili waombolezaji wataendelea kuwasili nyumbani kwa Mzee Dkt. John Samweli Malecela Kilimani Dodoma ambapo siku ya Jumatatu mwili utawasili nyumbani Kilimani Dodoma saa nne asubuhi ambapo itafanyika sala fupi na baada ya hapo mwili utaelekea Kanisa la Anglicana Dodoma
ambapo mwili utaelekea Mvumi kwa ajili ya maziko.

Dkt. Mwele alifariki dunia Alhamisi Februari 10, 2022 jioni mjini Geneva, Uswisi wakati akipatiwa matibabu.