November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Uzalishaji wa dhahabu Mkoa wa kimadini Kahama waendelea kushika kasi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Afisa Madini Mkazi Kahama, Mhandisi Jeremiah Hango amesema kuwa Uzalishaji wa dhahabu umeongezeka kwa kasi kutokana na usimamizi mzuri, sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya Madini.

Mhandisi Hango aliyasema hayo tarehe 14 Februari, 2022 baada ya timu ya Wataalam kutoka Tume ya Madini na  Imaan Media kutoka Morogoro kutembelea mgodi wa Bulyanhulu uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala na kujionea shughuli za uchenjuaji wa

Alisema kuwa, kuanzishwa kwa masoko ya madini nchini hasa kwenye mkoa huo wa kimadini kumekuwa na mafanikio makubwa kutokana na shughuli za biashara kufanyika sokoni.

“Tumekuwa tukivuka lengo kwenye ukusanyaji wa maduhuli ambapo kwa miezi sita iliyopita kwa mwaka wa fedha 2021/2022 tumekusanya asilimia 110 kupitia shughuli mbalimbali za uzalishaji wa dhahabu,”alisema Mhandisi Hango.

Naye Mkuu wa Uchenjuaji wa dhahabu kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Mhandisi Enock Edward alisema kuwa usalama, utunzaji wa mazingira na mabaki yatokanayo na kemikali ni kipaumbele kikubwa kwa usalama wa Wafanyakazi.