Na Hadija Bagasha, Tanga,
Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema wizara ya afya itawapima utendaji wao wa kila siku waganga wakuu na waganga wafawidhi nchi nzima wa hospitali za serikali kwa mambo sita kulingana na utendaji wao wa kila siku.
Ummy aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo cha Afya Makorora Jijini Tanga ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea eneo la kuhifadhiwa dawa kwenye kituo hicho ambapo atawapima watoa huduma zao kuanzia Hospitali za Taifa, Rufaa,Mikoa,wilaya,Zahanati na Vituo vya Afya.
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea kituo cha afya cha Makorora jijini Tanga.
ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea
Waziri Ummy aliyataja mambo hayo kuwa ni mapokezi ya mgonjwa na lugha na hiyo ni kutokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wagonjwa ambao wamekuwa wakipatiwa na wataalamu wa afya pindi wanapofika kupata matibabu.
Jambo la pili amesema watawapima katika wagonjwa 100 waliofika ni wangapi waliochukuliwa rekodi yao, jambo la tatu watakaloangalia ni historia ya mgonjwa kama amefanyiwa uchunguzi wa kutosha kulingana na tatizo alilonalo.
Jambo la nne ni watakaliangalia ni mgonjwa kama amepatiwa vipimo vyote anavyotakiwa kupatiwa , jambo la tano ni kuangalia kama mgonjwa amepatiwa dawa anayostahili kupata katika hospitali huku jambo la sita watakaloangalia ni kwamba mgonjwa ametumia muda gani kupata huduma.
Waziri Ummy amesema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikishawatanzania wanapata huduma bora za afya na si bora tu huduma kwa kuangalia maeneo hayo 6.
“Kipaumbele cha awamu ya sita kitakuwa ni kuwekeza kwenye huduma bora za afya tunataka kutofautisha hospitali na waganga wa kienyeji ikumbukwe mganga wa kienyeji yeye hapimi afya lakini hospitali ni tiba na huduma za kiuchunguzi kitaalamu, ” amesisitiza Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema baada ya kutembelea kituo cha Makorora wamebaini mambo mawili ikiwemo changamoto ya bohari ya dawa licha ya wao kuwa na mpango mzuri wa kutoa huduma kwajili ya watoto wachanga wanaozaliwa na uzito pungufu.
“Wameorder vifaa MSD toka mwaka jana 2021 na vifaa vyenyewe siyo vingi cha kushangaza mpaka leo MSD ameshindwa kusema vifaa kama anavyo au hakuna hii ndio maana juzi katika, maelezo yangu nilisema tutaangalia mnyororo mzima wa dawa katika ununuzi, usambazaji na usafirishaji wa dawa kuanzia ngazi ya kituo mpaka MSD, “amebainisha Waziri Ummy.
Wakati huo huo Waziri Ummy amepiga marufuku hospitali zote nchi nzima kuacha kuwatoza fedha kina mama wajawazito nchi nzima na badala yake huduma zote zinazopatikana wapatiwe bure ikiwa ni pamojana huduma ya Ultra sound pamoja na watoto wachanga zitolewe bure ili kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga.
“Mnapoweka kikwazo cha elfu 40 kwa jili ya vipimo kina mama wengi tutawakosa nyie wenyewe mnajua hudhurio la kwanza la mama mjamzito kliniki ni chini ya asilimia 50 wajawazito wengi wanashindwa kuja kliniki mapema kwasababu ya michango na matizo yasiyokuwa namaana tunayawatoza hii ni sera ya afya hatujaifuta na hatujaibadilisha, “amesisitiza Waziri Ummy.
More Stories
Serikali yahimiza wananchi kutembelea vivutio vya utalii
Magunia ya kufungia tumbaku yakamatwa
Madereva 16,Mwanza wafungiwa leseni ya udereva