Na Mwandishi wetu,Timesmajira,Online
MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amempongeza Rais Samia Suluhu kwa kuteuwa mawaziri, manaibu mawaziri na makatibu wakuu ambapo amesema kuwa ni wazi Rais Samia amekusudia kuboresha maisha ya watanzania.
Akizungumza leo Januari 11, mbunge huyo amesema kuwa viongozi hao wapya ni wazi kuwa ni wachapakazi na wazalendo ambapo wataweza kwenda na kasi katika kutatua changamoto za wananchi.
“Rais Samia ameendelea kuthibitisha kwa vitendo anayo nia ya dhati ya kuboresha maisha ya Wananchi kwa kuteua wasaidizi wachapakazi, Wazalendo na Vijana wengi ambao binafsi naamini watakwenda speed kukimbizana na matatizo na changamoto za wananchi” amesema Mariam Ditopile.
Aidha, amewapongeza viongozi hao kwa kuaminiwa na kuteuliwa katika nafasi hizo ambapo amesema kuwa “Nichukue Nafasi hii kuwapongeza Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu walioaminiwa na kuteuliwa.”
Amesema Watanzania wana imani kubwa na Serikali ya Rais Samia ambapo katika kipindi kifupi uchumi umeimarika, huduma za jamii zimeendelea kuboreshwa na kipato cha mtu mmoja mmoja kinaongezeka
More Stories
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato
Wambura asikitishwa na makundi CCM Nyakato