Na Martha Fatael, Siha, TimesMajira Online
SERIKALI mkoani Kilimanjaro imetaka asasi za kifedha kusaidia wajasiriamali wadogo kupata mikopo yenye Riba nafuu badala ya kuwaacha waangukie katika mikopo Umiza inayoua mitaji yao.
Mkuu wa mkoa huo Steven Kagaigai amesema hayo wakati anazungumza na watumishi wa Uchumi Commercial Bank (UCB) wilayani Siha kwenye maonesho ya bidhaa katika miaka 60 ya Uhuru iliyofanyika viwanja vya CCM wilaya ya Siha.
Ametaka UCB pamoja na asasi nyingine kutengeneza mifumo rafiki kwa wajasiriamali na wakulima wadogo ili kukuza mitaji yao badala ya kuwaacha wafilisike.
Kagaigai amesema kwa miaka 60 ya Uhuru Taifa limepiga hatua kubwa za maendeleo katika sekta za Elimu, Afya, Kilimo, Nishati na miundombinu ya barabara hivyo ni wajibu wa wadau wa maendeleo wakaunga mkono juhudi za serikali.
Mapema msimamizi wa Tawi la UCB Ltd,James Kileo amesema benki Inatoa huduma za aina mbalimbali na tayari imewezesha wajasiriamali zaidi ya 1000 mkoani hapa ambao baadhi wamefungua viwanda vidogo na kuajiri watu wengine.
Naye mkuu wa wilaya ya Siha, Thomas Apson amewataka wananchi na wajasiriamali kuchangamkia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ya wilaya lakini waombe fedha nyingi na siyo kidogo kama wafanyavyo Sasa.
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti