November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naibu Waziri wa Maliasili awataka askari uhifadhi kufanya kazi zao kwa uadilifu

Judith Ferdinand,Simiyu

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amewataka askari wa uhifadhi nchini kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu ili kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa manufaa ya Taifa.

Ameyasema hayo jana katika kikao chake na Askari Uhifadhi alipotembelea Hifadhi ya Pori la Akiba Kijereshi lililoko wilayani Busega mkoani Simiyu.

Pia Masanja amewataka askari hao kushirikiana na wananchi katika kukabiliana na tatizo la tembo.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Maafisa na Askari Uhifadhi kutoka Pori la Akiba Kijereshi na Kikosi dhidi ya Ujangili kutoka Bunda na Mkoa wa Mwanza.

Baadhi ya Maafisa na Askari Uhifadhi kutoka Pori la Akiba Kijereshi na Kikosi dhidi ya Ujangili kutoka Bunda na Mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao alipotembelea Hifadhi ya Pori la Akiba Kijereshi lililoko Wilayani Busega mkoani Simiyu.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja akizungumza na Maafisa na Askari Uhifadhi alipotembelea Hifadhi ya Pori la Akiba Kijereshi lililoko Wilayani Busega mkoani Simiyu. Kushoto ni Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Ziwa Laurent Katakweba na Meneja wa Pori la Akiba Kijereshi, Lusato Masinde (kulia)