November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Angeline Jimbo Cup kuanza kutimua kesho,milioni 24 kutumika

Na Judith Ferdinand,TimesMajira Online,Mwanza

MASHINDANO ya Angeline Jimbo Cup 2021, ambayo yatashirikisha timu 19, kutoka kata zote zilizopo jimboni Ilemela yanatarajia kuanza kutimua vumbi Agousti 20,mwaka huu,huku jumla ya milioni 24,zitatumika katka mashindano hayo.

Mashindano hayo ambayo yalianzishwa rasmi mwaka 2016, na Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula,kwa lengo la kuinua vipaji kupitia michezo jimboni humo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu hizo zitakazo shiriki mashindano hayo, Mbunge wa Jimbo la Ilemela,Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula alisema
kutokana na yeye kuwa mwanamichezo pamoja na kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ndio maana alianzusha mashindano hayo.

Dkt.Angeline,amesema michuano ya msimu huu imeboreshwa zaidi kupita michuano iliyopita kuanzia kwenye zawadi wameboresha kutoka mshindi wa kwanza hadi wa nne msimu huu.

Amesema,mshindi wa mashindano hayo kwa msimu huu atajinyakulia zawadi ya milioni 2 mshindi wa pili milioni 1.5, mshindi wa tatu milioni 1 huku mshindi wa nne atapata 500,000.

Pamoja na zawadi hiyo mshindi wa kwanza hadi wa tatu watapewa kombe, jezi seti moja na mpira huku mshindi wa nne atapewa jezi na mpira tu ambapo zawadi za washiriki bora zikitolewa pia.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela,Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula( wa kwanza kulia),akimkabidhi vifaa vya michezo kiongozi wa timu moja wapo kati ya timu 19 kutoka kata zote zilizopo jimboni Ilemela,zitakazo shiriki mashindano ya Angeline Jimbo Cup yanayotarajia kuanza kutimua vumbi Agousti 20,mwaka huu.picha na Judith Ferdinand

Mratibu wa Mashindano hayo,Katibu wa Chama cha Mpira Wilaya ya Ilemela Almasi Moshi Almasi,amesema michuano hiyo itachezwa kwa mtindo wa makundi,manne ambayo yatatumia viwanja vya Buswelu, Kona ya Bwiru, Saba Saba na Bugogwa.

Amesema,jumla ya timu 19,kutoka kila kata jimboni Ilemela zinatarajia kushiriki mashindano hayo ambayo yamekuwa yakiongezeka hamasa kila mwaka huku ukiwa ni msimu wake wa tatu toka yaanze.

Kwa Upande Ofisa Michezo wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Kizito Bahati, amesema suala la matibabu ya kwanza kwa wachezaji watakaoumia limezingatiwa,waamuzi(refals) wa kusimamia sheria 17,wapo hivyo timu shiriki zipambane uwanjani ili zipate ushindi.