Na Judith Ferdinand,TimesMajira Online,Mwanza
BAADA ya mlipuko wa kwanza wa virusi vya Covid-19 kuingia nchini hapa mwaka 2020,Serikali ilizifunga shule zote ili kuwalinda na kuwakinga watoto wote dhidi ya virusi hivyo.
Hali hiyo ilisababisha kwa kipindi cha miezi mitatu watoto kushindwa kuhudhuria masomo shuleni,jambo ambalo lilichangia kwa namna moja au nyingine baadhi ya watoto kusahau masomo.
Licha ya changamoto hiyo Serikali kupitia Wizara ya Elimu ilitoa muongozo wa watoto kusoma kupitia vyombo vya habari pamoja na majaribio yaliyokuwa yanatolewa na walimu shuleni kwa wazazi wa watoto kuyafuata na kuyarudisha mara baada ya kumaliza kufanya.
Hata hivyo njia hiyo kwa namna moja au nyingine ilisaidia ila siyo kwa kiwango kikubwa kutokana na mfumo wa elimu ambao upo nchini na uliozoeleka kwa wanafunzi na walimu kukutana pamoja ana kwa ana na kuweza kufundishana,kuuliza maswali na kuelekezana.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala, akizungumza na Majira alielezea namna Wilaya hiyo ilivyojitahidi kurejesha watoto katika hali ya kawaida ya uelewa wa masomo mara baada ya likizo ya Corona na shule kufunguliwa.
Masala,amesema wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya nchi,hivyo changamoto zilizojitokeza katika taifa kutokana na COVID-19, kwa mwaka 2020 ndio zilizoikumba na Wilaya ya Ilemela.
Amesema,miongoni mwa changamoto iliojitokeza kipindi cha Covid-19 ni suala la utoaji elimu kwa sababu muda mrefu watoto walikaa nyumbani hivyo mawasiliano kati ya walimu na wanafunzi kidogo yalikuwa magumu.
Pia amesema,katika kukabiliana na hali hiyo ipo mikakati ambayo wilaya walijiwekea kupitia idara yao ya elimu msingi na sekondari ambazo zilitenga muda wa ziada mara baada ya shule kufunguliwa.
Ambapo waliamua kuwaweka shuleni watoto kwa muda mrefu kwa kuwapa masomo ya ziada lakini pia kwa kuongeza muda wa kutoa vipindi ili kufidia muda ambao umepotea kipindi ambacho wanafunzi walikaa nyumbani takribani miezi mitatu.
Kwaio mara baada ya shule kufunguliwa walikaa na walimu kupitia viongozi wenzake walionitangulia,wakaweka makubaliano ya kuongeza muda wa ziada,kutoka muda wa kawaida wa Serikali kwenda wa ziada.
Lakini pia hata siku za mwisho wa juma(weekend),zimetumika skwa ajili ya kuwasaidia watoto,mazoezi pia ya mitihani na mazoezi ya kielimu imefanyika na mitihani ya ujirani mwema.
“Kwa kiasi kikubwa iliondoa hiyo changamoto cha kutoathiri matokeo ya watoto wetu na ukiangalia matokea angalau kidogo watoto walikuwa hawajapata hiyo changamoto ya kufeli mitihani yao,hii ni kutokana na jitihada za kuziba pengo ambalo watoto wetu walilipata bila ya kukutana na walimu kwa ajili ya kusoma,”amesema Masala.
Naye mmoja wa wananchi wa mtaa wa Nyamanoro Mashariki Agnes Lucas,amesema kipindi cha likizo ya COvid-19, watoto wengi walishindwa kusoma kwa sababu ilikua tofauti na likizo nyingine ambayo licha ya shule kufungwa lakini wanapata fursa ya kusoma masomo ya ziada(tution).
Agnes amesema,hali hiyo kwa namna moja amma nyingine baadhi ya watoto walirudi nyuma kitaaluma kwa sababu siyo wazazi wote walikua na uwezo wa kuwafuatia watoto wao mitihani na kuirudisha.
Amesema,siyo familia zote zinalikuwa na runinga,hususani za vijijini pia jamik pia ilikua haina uelewa wa namna ya kuwasaidia watoto wao kujisomea kulingana na tamaduni iliozoeleka ya kutegemea walimu tu.
More Stories
Dkt.Tulia ashiriki ibada, asisitiza waumini kushiriki uchaguzi serikali za mitaa
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia