November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanafunzi Chuo cha Kumbukubu Mwalimu Nyerere wafurahishwa na mafunzo ya uongozi na maadili

Na Rose Itono,TimesMajira Online, Dar

WANAFUNZi wabunifu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wamesema mafunzo ya uongozi na maadili wanayopewa chuoni hapo yamewajenga kuwa imara katika shughuli zao za baadaye

Wakizungumza kwenye Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja,ya walisema mafunzo ya uongozi na maadili wanayopewa yamewawezesha kuwa imara katika utekelezaji wa shughuli zao mbalimbali zikiwemo bunifu
.

Jonas Katial mwanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya ya Mwalimu Nyerere akitoa maelezo kuhusiana na ubunifu wake wa mfumo wa umwagiliaji unaoweza kufanyika pasipo mkulima kuwepo shambani.Picha na Rose Itono

Jonas Katial mmoja wa wanafunzi aliyehitimu diploma ya TEHAMA chuoni hapo amesema ameamua kubuni mfumo utakaomuwezesha mkulima kumwagilia
shamba bila kuwepo ili kumpunguzia muda wa kukaa shambani pasipo kufanya shughuli nyingine za kujiongezea kipato.

Amesema kwa kutumia mfumo huu mkulima atakuwa anapata taarifa zote za umwagiliaji zinazoendelea shambani kupitia simu yake ya mkononi.

“Mfumo huu wa umwagiliaji unajiongoza wenyewe baada ya kupima udongo, udongo ukiwa mkavu pampu inawaka yenyewe
na kuanza kumwagilia shamba na wakati huo kitendo hicho kinapoendelea mkulima atapata ujumbe wa kumtaarifu kuwa shamba lake linamwagiliwa, “amesema Katial na kuongeza kuwa mara udongo utakaoloa maji ya kutosha mkulima atapata taarifa na pia

mfumo huu wa umwagiliaji haubagui chanzo cha maji na ni rahisi kuutumia.