Na Mwandishi wetu,timesmajira,Online
SHIRIKA la ndege la Emirates imesema itaendelea kuongeza huduma zake kwa ufanisi hususani katika kushughulikia mahitaji ya wasafiri wake hasa katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Uviko-19.
Pia shirika hilo limesema linaendelea na mpango wake katika kushughulikia mahitaji ya wasafiri katika utunzaji na uhifadhiji wa mizigo yao unaendelea kuwa mzuri kwa kuhakikisha wateja wao wanakuwa huru na safari zao.
Taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Emirates jana,ilisema shirika hilo linaendelea kuhakikisha linatoa huduma nzuri kwa wateja wao.
Aidha imesema shirika hilo linaendelea kulinda afya za wateja wao hususani katika kipindi hiki cha Uviko-19 katika kuhakikisha hali ya usalama inakuwepo katika kila hatua ya safari za abiria wake.
“Wasafiri bado watahitajika kupata chanjo kamili angalau siku 14 kabla ya tarehe ya kusafiri au kuwasilisha karatasi maalum waliyopima COVID-19 ambayo uchukuliwa kati ya masaa 48 hadi 96 kabla ya kuwasili, kulingana na marudio,”imesema
Aidha taarifa hiyo imesema wakati nchi zinapunguza vikwazo vya kusafiri kwa watalii hususani kwa watanzania ambao wamepata likizo ya mapumziko ya kwenda katika nchi ya Dubai, Uturuki, Maldives, Shelisheli na Urusi ambapo wameondoa hitaji la kuweka karantini wakati wa kuwasili kwa watu ambao sio wakaazi wan chi hizo.
Imesema Kila wiki shirika lao linatoa ndege za Emirates ambazo ni salama kwa abiria na zenye kuwabeba wateja mbalimbali ikiwemo familia.
“Wasafiri wamekuwa wakitafuta vitu vipya vya kujifunza hivyo wakikaa ndani ya ndege za Emirate wanakuwa wapo huru katika kujifunza vitu vingi,”imesema
More Stories
Mwalimu adaiwa kumfanyia ukatili mwanafunzi
NAOT watakiwa kuendana na viwango vya ukaguzi
Rais Samia kuzindua mfuko wa kuendeleza kazi za wabunifu