November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

13 washinda, wajinyakulia mil.85/-

Na Mwandishi wetu,TimesMajira Online, Dar

MTANDAO wa Asasi za Huduma za Kifedha (TAMFI) mwishoni mwa wiki wamewatakangaza washindi 13 waliojinyakulia jumla ya Sh milioni 85 katika Tuzo za Ujasiriamali Mdogo za Citi (CMA).

Katika hafla iliyofanyika kwa njia ya mtandao, ushindi wa kwanza katika tuzo hizo ilienda kwa Ruth Gidion Magawa ambaye anamiliki kiwanda kidogo cha kuchakata maziwa alioyejinyakulia dola 7,500 na tuzo ya pili ilenda kwa, Daudi Marko Simfuke mwenye kiwanda cha zana za kuchakata bidhaa za kilimo ambaye alipata dola 6000.

Mshindi wa tatu wa dola 4,000 alikuwa ni Joyce Robert Kalamageambaye ana endesha duka la dawa, zahanati na dukakuu dogo.

Washindi wengine ni Victoria Kavula, Suma Mwanjabiki, Daniel Mpanduzi,Aristides Kenzio,David Mugitu,Richard Kashinje, Tabitha Gityamwi,.Hellena Sailas na Salum Msengi.

Washindi hao 13 walitokana na idadi ya watu 24 walioingia raundi ya mwisho kati ya washiriki 350 waliosajiliwa awali.

Tuzo hizo zimeendeshwa nchini mara ya 4 kwa ushirikiano kati ya Citi Foundation na TAMFI. Tuzo za mwaka huu zimeunganishwa na Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (UN SDG).

Tuzo hizo ni sehemu ya mwendelezo wa benki ya Citi kwenye eneo la mikopo midogo midogo kuwasaidia wajasiriamali wadogo kwa kupitia utoaji tuzo za Citi kwa kila mwaka.Mkakati huo ulianzishwa mwaka 2005 kwa kutambua michango ya wajasiriamali wadogo na pia michango ya asasi zinazotoa huduma za kifedha kwenye maeneo yao.

Mwakilishi wa majaji Prof Jones Kaleshu, amesema kwamba katika msimu huu wameona mabadiliko makubwa katika ufanisi wa tuzo na pia dhamira safi za washiriki kujiinua kitija.

Amesema tuzo hizo zimeinua molariya wajaioriamali wadogoa ambao wanahitaji msukumo wa pekee kuondojka pale walipo kwa sasa.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji MKuu wa Citibank Tanzania, Geofrey Mchangila, program hiyo (CMA) imelenga kutambua mchango wa wajasiriamali hao katika kuimarisha kipato chao kaya zao na taifa kwa ujumla.

Amesema tuzo hizo zimezingatia wajasiriamali wabunifu wanaokwenda sambamba na malengo ya maendeleo endelevu ya umoja wa mataifa.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TAMFI,Altemius Millinga, ambaye apia ni Mkurugenzi mtendaji wa Yetu Microfinance Bank PLC, amepongeza program hiyo na kusema inashughulikia kuwapatia mitaji watu wasiokuwa na uwezo.