November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wenye ualbino waiomba Serikali, wadau msaada

Na Esther Macha,TimesMajira Online, Mbeya

WATOTO wenye ualubino mkoani Mbeya,wameiomba Serikali na wadau wengi kuwasaidia vifaa maalum vitavyowasaidia kuhimilivu mionzi ya jua.

Kupatikana kwa vifaa hivyo ambavyo vitakuwa rafiki kwao kutakuwa msaada kwao kwani wanaweza kuchangamana na wenzao mashuleni wakati wa zoezi la unawaji mikono katika kukabiliana na Ugonjwa wa Corona.

Imeleezwa kuwa licha ya kuwepo kwa vitakasa mikono lakini bado lipo tatizo kwa watoto wenye ualbino kushindwa kumudu foleni wakati wa kunawa mikono kutokana na hali walinayo ambayo wanashindwa kumudu jua kali kutokana na hali walizonazo.

Akizungumza na TimesMajira Online jana Katibu wa Chama Wenye Ualubino Mkoa wa Mbeya ,William Simwali amesema kuwa pamoja na changamoto hiyo kwa watoto wenye ualubino waliopo shuleni pia kuna gharama kubwa za barakoa ambazo wazazi wa watoto hao walio wengi hawawezi kununua mara kwa mara.

“Watoto hawa wenye ualubino wana changamoto kubwa mtoto mwenye ualubino hawezi kusimama juani wakati wa kusubiria kunawa mikono kama unavyojua ndugu yangu kwenye mashule yetu haya watoto ni wengi hivyo mpaka foleni imkute wakati kashaumia ,ushauri wangu kwa serikali na wadau iangalie namna ya kutenga maeneo kwenye shule ili kusaidia kundi hili “amesema Katibu.

Hata hivyo Simwali aliomba serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo walipe kipaumbele kundi hilo katika kupambana na ugonjwa hatari wa corona kama wanavyosaidia makundi mengine .

Akielezea zaidi Katibu huyo amesema kuwa Kwa kushirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali la DAI kwenye mradi wake wa inua vijana Tanzania waliweza kuwezeshwa mafunzo ya kupambana na ugonjwa wa corona wapatao 20 pamoja na vijana wengine wenye ulemavu 30.

“Tunaaminiu kwamba mafuynzo haya yatasadia kwa kiasi fulani ingawa bado ipo changamoto kwa hawa watoto waliopo mashuleni tunaomba sana serikali na wadau walione hili na hapa ni mjini hatujui hali ikoje huko vijijini ambako ndiko kuna watoto wengi wenye ualubino “amesema.

Aidha amebanisha kuwa shirika lisilokuwa la kiserikali la SHIVYAWATA Mkoa wa Mbeya na Child Support Tanzania limekuwa likifanya jitihada za mara kwa mara za kutoa elimu ingawa bado nao wanahitaji kusaidiwa ili waweze kufikia kundi kubwa la watoto.

“Mkoa wetu wa Mbeya bado hatujaweka sawa idadi ya watoto wenye ualubino wanaosoma tunaendelea na taratibu ingawa kwa watu wazima wenye ualubino tunao 210.

Aidha Katibu huyo aliomba kwa serikali kuonaq umuhimu wa ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika kupanga mambo yanayofanyika katika jamii.

Pia ameshauri serikali ione umuhimu wa kitengo cha ustawi wa jamii katika halmashauri kuwa idara kamili badala ya kuwa chini ya mganga mkuu wa wilaya matokeo yake maswala ya watu wenye ulemavu hayapewi umuhimu stahiki.

Akizungumzia na gazeti hili mkazi wa Isyesye Jijini Mbeya ambaye ni mwanamke mwenye Ualubino , Upendo Ngodya amesema kuwa kumekiwa na changamoto kwa watoto wenye ualubino kipindi hichi cha wimbi la tatu la Corona ni kukosa vifaa vya kujikinga na Corona,watu kutowajali kama watoto wengine.

Aidha mkazi wa uwanja wa ndege ya zamani ,Gwantwa Mwalyaje ambaye pia na ni Alubino amesema kuwa wana ombi kwa serikali kuweka kipaumbele kwa watoto yatima wenye ualubino waliopo mashuleni wapewe vikinga jua wa kunawa mikono na serikali itoe msaada wa vifaa na elimu ya kutosha kuhusu wimbi la tatu la Corona.