November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mashine ya kuchanganya chakula kuwarahisishia wafugaji

Na Penina Malundo,TimesMajira Online

KUTOKANA na wafugaji wengi hapa nchini kukabiliwa na changamoto ya kushindwa kuchanganya vyakula vya mifugo kwa uwiano, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) wameamua kuja na mashine hiyo ili kumaliza shida hiyo.

Akizungumza katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar Salaam, Daktari wa Mifugo, Ladslaus William amesema wameamua kuja na ubunifu huo kutokana na changamoto inayowakabili hasa wafugaji wa kuku kwenye kuchanganya chakula.

Amesema, wakati wa kubuni mashine hiyo walilenga kumsaidia mfugaji kufanya shughuli zake kwa usahihi ambapo pia kutamuwezesha kuona manufaa ya kile anachokifanya.

“Ni vema wafugaji wakaelimishwa umuhimu wa kuipa chanjo Mifugo yao,namna ya kupata Mbegu bora, namna ya mwisho yanayostahili kwa Ng’ombe au kutengeneza vyakula sahihi kwa mifugo wanayohitaji kulisha kama kuku ili wafugaji kwa faida zaidi,”.

“Tukitegemea vyakula vinavyotoka kiwandani peke ake vinakuwa na gharama kubwa tuweke tija kwa wakulima na wafugaji kwani inakuwa gharama ndogo kwao,wajitahidi kuangalia ni namna gani ya utengenezaji wa chakula cha Mifugo,” amesema amesema Dkt. William.

Amesema, kupitia maonesho hayo wananchi wafike banda la VETA kuona na mashine hiyo na wale wafugaji wa kuku kupata mashine na kazi ya VETA kutoa sualuhu kwa jamii katika kurahisisha katika nynzo za kufanyia kazi hasa uchumi wa sasa unaokwenda na Teknolojia.

“VETA Kazi yetu ni kutatua changamoto kwa wananchi katika Sekta ya ufugaji kwenda kisasa kwa kuweza kupata kuku wenye ubora na kuingia katika soko bila kukutana na vikwazo vinavyotokana na lishe,” amesema Dkt. William.

Lakini pia Mamlaka hiyo imewataka wafugaji kuwa na mazoea ya kutembelea wataalamu wa mifugo na maafisa ugani waliopo katika Vijiji na Kata zao kupata elimu sahihi juu ya ufugaji wa mifugo yao.