November 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakulima washauriwa kujiunga kwenye vikundi ili kutambulika

Na Mwandishi wetu, TimesMajira, Online

WITO umetolewa kwa Wakulima nchini kujiunga katika vikundi ili watambulike kisheria na kupata fursa za mikopo za kuboresha shughuli zao.

Ofisa Mwandamizi Masuala ya Masoko na Uendelezaji wa Biashara kutoka benki ya biashara ya Zanzibar (PBZ), Mohamed Khakis Ismail akizungumza katika Maonyesho ya 45 ya kimatafa ya biashara (DITF) yanayofanyika katika viwanja vya Julias Nyerere Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika Maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (DITF) ambayo yanafanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam
Ofisa Mwandamizi Masuala ya Masoko na Uendelezaji wa Biashara kutoka benki ya biashara ya Zanzibar (PBZ), Mohamed Khakis Ismail amesema benki hiyo katika kumkomboa mkulima imekuwa ikitoa mikopo kwa makundi ya wakulima wa korosho na karafuu.

Amesema lengo la kutoa mikopo hiyo ambayo ina unafuu ni kuwawezesha wakulima ili waweze kuboresha kilimo chao zaidi, kukuza uchumi wao na wa nchi kwa ujumla,

Alitoa wito kwa kwa vikundi mbalimbali kuchangamkia fursa katika kipindi hiki cha maonyesho ya sabasaba kutembelea banda lao ili kupata elimu ya huduma mbalimbali za kifedha kwa ajili ya kuendeleza miradi yao.

“Maonyesho ya Sabasaba ni fursa kubwa sana, wanatakiwa kuichangamkia, wakija hapa PBZ watafahamu aina ya mikopo wanayotakiwa kuchukua na niwashauri waondoe ile dhana ya kuogopa kuchukua mikopo kwenye taasisi za kibenki bila kufika na kupata elimu sahihi, wasisikie yale wanayoambiwa, wakumbuke kwamba uchumi wao na wa nchi utakuwa bora kwa kufanya kazi kwa bidii kama Rais Samia Hassan Suluhu anavyotusisitiza kila mara, “amesema Ismail

Nakuongeza kuwa”Miongoni mwa huduma ambazo tumekuwa tukitoakwa ajili ya kusaidia makundi mbalimbali ya pande zote za muungano ni pamoja na kutoa mikopo nafuu kwa vikundi vya vyama vya wakulima na masoko (AMCOS)ambavyo vinatambulika kisheria.

Alibainisha kuwa benki hiyo mpaka sasa imekuwa ikitoa mikopo kwa makundi ya wakulima wa korosho na karafuu na ni nafuu kwa sababu lengo lake ni kutaka viboreshe kilimo chao zaidi, kukuza uchumi wao na wa nchi kwa ujumla

Akizungumzia kuhusu huduma za kibenki zinazotolewa na benki hiyo katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara zimechangia kwa kiwango kikubwa kutangaza umuhimu wa Muungano.

Amesema faida ambazo zimeletwa na uwapo wa Muungano huo ikiwamo benki hiyo ya PBZ ambayo imekuwa ikitoa huduma katika mikoa mbalimbali katika pande zote za muungano na hivyo kuchagiza kuinua uchumi wa wananchi kutoka katika makundi tofauti yaliyopo katika muungano huo.

“Tunafurahi na tunafarijika kwamba muungano una faida kubwa na sisi kama PBZ tumetumia huduma zetu kuendelea kuutangaza hasa katika kuhakikisha wananchi wote wananufaika kupitia taasisi hii ya fedha kuinua uchumia wao na wa nchi kwa ujumla,”amesema Ismail

Amesema ili kupanua wigo wa utoaji wa huduma zao zaidi, wamejipanga kujitanua katika mikoa yote ya pande zote za muungano.

Ismail amesema kwa sasa benki imekuwa ikito huduma Zanzibar na katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, na Mbeya.