November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

WoteSawa wataka changamoto za watoto zipatiwe ufumbuzi

Na Judith Ferdinand, TimesMajira,Online Mwanza

PAMOJA na jitihada nyingi za Serikali za kulinda haki za watoto, lakini bado kuna changamoto ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi na wadau, jamii, vyombo vya kisheria pamoja na Serikali kwa ujumla.

Akizungumza na Majira wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Shirika la WoteSawa, Angela Benedicto, amesema wamemsikia Rais Samia Suluhu Hassan, alivyokuwa anahutubia vijana mkoani hapa akieleza kuwa elimu ya kidato cha nne kuwa ni elimu ya msingi.

Angela amesema licha ya elimu hiyo kuwa ni msingi, lakini bado wanaona watoto wameshindwa kufika kidato cha nne kwa sababu ya kutumikishwa kazi mbalimbali ikiwemo za ndani na mitaani.

Aidha, amesema haki ya elimu iendelee kuzingatiwa kwa sababu inatolewa bure na wazazi ambao hawafanyi hivyo wachukuliwe hatua za kisheria,” amesema Angela.

Mkurugenzi wa Shirika la WoteSawa, Angela Benedicto akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambayo kimkoa yalifanyika katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.

Amesema wito wake kwa wadau kama wao na Serikali kuendelea kutekeleza na kusimamia sheria na miongonzo ya watoto ambayo inakuwepo pamoja na taifa hili lisimamie mikataba na makubaliano ya kimataifa ambayo yamewekwa katika ulinzi wa mtoto.

Pia amesema, jamii kwa umoja kuhakikisha kila mmoja anajukumu la kumlinda mtoto na wanapooana vitendo ambavyo siyo vizuri vya ukatili wa kingono na vingine vyote kwa watoto waweze kutoa taarifa sehemu husika na watu hao waweze kuchukuliwa hatua.

Huku masuala ya watoto yanapofikishwa mahakamani basi mahakama iweze kutoa hukumu kwa wakati kwa sababu wameona watoto wengi wanatendewa ukatili lakini mashitaka yanaenda taratibu hadi inafika hatua watu wanakata tamaa.

“Leo ikiwa siku ya kuambukiza ya mtoto wa Afrika,tunakumbukia kwamba tarehe 16 Juni watoto nchini Afrika Kusini waliweza kuandamana wakidai mambo mbalimbali ikiwemo elimu na masuala mazima ya ustawi wao, kwa muda ambao tumekuwepo tangu 2012 mpaka sasa watoto karibia 600 tumeweza kuwaokoa katika vitendo vya ukatili na kuweza kuwarejesha nyumbani,”amesema Angela.

Ofisa mradi wa usawa kwa wanawake wafanyakazi wa nyumbani kutoka shirika la WoteSawa, Demitila Faustine amesema shirika hilo linajishughulusha na kutetea haki za watoto na wanawake wafanyakazi wa nyumbani na kupinga usafirishaji haramu wa watoto.

Ambapo wamekuwa wakiwajengea uwezo katika masuala ya kisheria,haki zao za msingi, mafunzo ya stadi za maisha pia wana makao kwa ajili ya kuishi