November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Ummy:Sijaridhiwa na usimamizi wa miradi ya afya Chemba

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira online,Chemba

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu,amesema kuwa hajaridhishwa na usimamizi wa miradi ya afya katika Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma hivyo waliohusika kutafuna fedha katika miradi hiyo atawatafuta popote walipo.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu,akizungumza na wananchi wa Hamai mara baada ya kukagua maendeleo ya Kituo cha Afya cha Hamai jana Wilayani Chemba Mkoani Dodoma.

Kauli hiyo ameitoa jana wilayani Chemba Mkoani Dodoma mara baada ya kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani humo ambapo ametembelea Shule ya Sekondari Chemba ,Hospitali ya Wilaya ya Chemba na Kituo cha Afya cha Hamai.

Waziri Ummy amesema ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chemba haukusimamiwa vizuri na ndio maana baadhi ya majengo bado hayajakamilika kwa asilimia 100 huku akihoji ni kwanini shilingi milioni 250 zilirudishwa hazina wakati ujenzi haujakamilika.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu,akitoa maelekezo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa mara baada ya kukagua maendeleo ya Kituo cha Afya cha Hamai ljana Wilayani Chemba Mkoani Dodoma.

“Lazima tukubali ujenzi haukusimamiwa vizuri hakukuwa na usimamizi mzuri wanaohusika na manunuzi hawakusimamia vizuri ndio maana milioni 250 zikarudi lakini hapa hakuna hata wagonjwa kwa sababu huduma muhimu hakuna,mna wagonjwa 1000 tu katika Hospitali ya Wilaya kuna shida,”amesema Ummy.

Amesema wote waliohusika na wizi katika miradi hiyo atahakikisha anawawajibisha hata kama wamehama katika Halmashauri hiyo.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu,akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chemba mara baada ya kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani humo ambapo ametembelea Shule hiyo ,Hospitali ya Wilaya ya Chemba na Kituo cha Afya cha Hamai jana Wilayani Chemba Mkoani Dodoma.

“Hii miradi imehujumiwa watu wametanguliza maslahi binafsi najua Mhadhisi aliondolewa ili watu wapige ninayomajina wameharibu wamepelekwa kwingine sasa hata kama ulihamishwa mimi hili siliachi,tukidhibitisha tunakupeleka mahakamani,”amesema.

Hata hivyo Ummy ametoa onyo kwa Watumishi wa TAMISEMI watakaoharibu katika kituo chake cha kazi hataruhusu ahame isipokua atamuwajibisha akiwa katika kituo chake cha kazi.

“Sitaruhusu mtumishi aharibu Chemba kisha ahamishiwe Kongwa, niwahakikishie kuwa ntamshughulikia akiwa hapa hapa Chemba na nikibaini ana hatia ntamchukulia hatua stahiki” amesisitiza Ummy.

Akiwa katika kituo cha afya cha Hamai,Waziri Ummy alipokelewa na wakazi wa vijiji vya Songolo na Hamai ambapo walidai huduma muhimu katika kituo hicho hazipatikani kama Xray,dawa,maji,ambulance,wodi ya wanaume pamoja na uzio.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dk.Binilith Mahenge ,akizungumza mara baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ambapo ametembelea Shule ya Sekondari ya Chemba ,Hospitali ya Wilaya ya Chemba na Kituo cha Afya cha Hamai jana Wilayani Chemba Mkoani Dodoma.

Katika hatua nyingine Mhe.Ummy amewataka Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kuchapa kazi kama awali na sio kukaa kusubiria uteuzi.

“Hali inayoendelea kwa viongozi hawa haileti afya, wengine hawafanyi kazi eti wanasubiria mkeka, hamuoni kuwa mnaonea wananchi kupata haki yao ya msingi ya kuhudumiwa” alihoji Waziri Ummy.

Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dk.Binilith Mahenge amesema atahakikisha maji yanapatikana katika Hospitali ya Wilaya na katika kituo cha afya cha Hamai.