Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online
WAKATI Askofu Getrude Rwakatare akitimiza mwaka mmoja tangu afariki dunia, familia yake imejivunia kuendelea kuwa imara na kuendeleza harakati za kutimiza ndoto zake zote.
Hayo yamesemwa na mtoto wake, Dkt. Rose Rwakatare wakati wa Ibada ya Maalum ya kumuombea na kumkumbuka iliyofanyika kwenye Kanisa aliloliasisi la Mlima wa Moto Mikocheni, Dar es Salaam.
Dkt. Rwakatare ambaye pia ni mwasisi wa shule za St Mary’s ambazo ni shule za kwanza kabisa za mchepuo wa Kingereza nchini alifariki dunia Aprili, mwaka jana.
Dkt. Rose Rwakatare amesema familia yao imeendelea kuwa na umoja, upendo na mshikamano na jitihada zinafanyika kuenzi mema yote aliyoyaacha na kutimiza ndoto zake hasa kutoa elimu bora kwa Watanzania.
Amesema shule alizozianzisha kwaajili ya kusaidia watoto wa Tanzania bado zinafanya vizuri kwenye matokeo ya kitaifa na wataendelea kuzisimamia kuhakikisha zinandelea kuwa juu kitaifa.
“Mchango wa Askofu Rwakatare umewagusa wengi na kila alichoanzisha kinaendelea vizuri na mbegu alizopandikiza kwa watoto, wasimamizi wa shule na waumini zinazidi kuwa nuru katika kuhakikisha maono yaliyobebwa na Mama yetu kipenzi yanaendelezwa,” amesema
Dkt. Rose alisema Kanisa na matawi yake, redio na shule zinaendelea vizuri na wamemefanya maboresho aliyokuwa anataka na ufaulu umekuwa ukipanda kila mwaka na matokeo ya darasa la nne la saba mwaka shule zimefanya vziuri sana,” amesema Dkt.Rose.
Pia amesema wataendelea kutoa huduma hizo kwa jamii ya Watanzania kuhakikisha wanajenga taifa imara la vijana makini kupitia elimu wacha Mungu na wenye kuleta tija kwa jamii.
Mtoto mwingine wa Askofu huyo, Mutta amesema mama yao aliwekeza kiroho na kutanguliza maombi kwa kila jambo na kuwaomba waumini na Watanzania wa ujumla kushirikiana katika kuhakikisha ndoto na maono ya Hayati. Askofu Rwakatare yanagusa wengi zaidi.
“Hakuna binadamu mkamilifu, tunaanguka mara nyingi nawaomba tusameheane kama Mama alivyokuwa anatufundisha,” alisema Mutta ambaye ni diwani wa Kata ya Kawe.
Naye Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba alisema, Askofu Rwakatare anakumbukwa kwa ujasiri na kujituma katika kuhakikisha jamii inapata huduma muhimu ikiwemo elimu na ibada.
“Kwa miaka 70 aliyoishi Mama Rwakatare alitumia vyema muda wake kwa kuwekeza kwenye vitu vinavyoendelea ikiwemo nyumba za ibada, redio, na shule.Tunamshukuru Mungu kwa ya Mama Rwakatare amethibitisha kuwa wanawake tunaweza,” amesema
Amesema, wakati wa uhai wake Askofu Rwakatare alikuwa na mchango mkubwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitumikia kwa vipindi kadhaa.
Amewapongeza watoto wake kwa kumuenzi Mama yao kwa kushirikiana na kushirikisha kanisa katika kuhakikisha maono yake yanazidi kuangaza kizazi kwa kizazi.
More Stories
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto
Kilo 673.2,dawa za kulevya zakamatwa Bahari ya Hindi