Na Penina Malundo,Timesmajira Online.
IMEELEZWA kuwa njia moja wapo ya kufanya mwanafunzi aweze kufaulu katika masomo yake ni pamoja na ushirikiano baina ya walimu na wazazi au walezi katika kuhakikisha wanangaliwa kwa weledi maendeleo ya Mwanafunzi na kwa ukaribu zaidi.
Akizungumza Dar es Salaam katika mahafali ya 14 ya kidato cha sita cha Shule ya Sekondari Huria ya Ukonga Skillful tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006 Mwasisi wa shule hiyo, Diodorus Tabaro amesema ushirikiano utakaofanywa na wazazi kwa watoto wao wanaosoma kwa kiasi kikubwa utaweza kuwaongezea ufaulu.
Amesema takribani wanafunzi 30 wa shule hiyo, wanatarajia kuhitimu mafunzo yao ya kipato cha sita katika shule hiyo, hivyo aliwataka kumtanguliza Mungu mwanzo wa mitihani yao hadi mwisho kwani shule yao imekuwa ikiamini katika Mungu.
“Shule yetu imekuwa ikimtengemea Mungu, mambo yote unayoyafanya, hivyo naahasa vijana hawa kuendelea kumtegemea Mungu wa kweli katika mitihani yao na kuamini wanafanya vizuri zaidi,” amesema.
Tabaro amesema shule yao imekuwa ikipokea wanafunzi ambao tayari wamekata tamaa na wengine wamekuwa hawamalizi shule, hivyo wamekuwa msaada mkubwa kwao katika utoaji wa elimu ambapo hadi sasa tayari wametoa wanafunzi waliomaliza vyuo vikuu mbalimbali wapatao 16.
“Unajua wanafunzi tunaowapokea ni wale waliokata tamaa ambao wengi wameishia njiani kimasomo na wengine waliokata tamaa, baada ya kufeli darasa la saba basi tunawachukua na kuwapa mafunzo maalumu ya kujitambua kwanza, halafu ndiyo wanaanza kusoma masomo ya darasani na hii ili kuwafanya akili zao sasa kuchangamka katika suala la masomo,” amesema.
Tabaro amewataka wazazi na walezi, kuhakikisha wanalipa ipasavyo karo au ada za watoto wao ili wasiwe kikwazo cha kukwamisha maendeleo ya mtoto kwenye safari yake ya masomo.
Katika mahafali hayo yalihudhuriwa na Msimamizi Mkuu wa shule zilizopo chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Baraka kionywaki huku mgeni rasmi akiwa
Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Sayansi ya Jamii, Dkt. Simon Mtebi ambaye amewataka wanafunzi hao kuondoa hofu kipindi chote cha mitihani na kuhakikisha wanamtanguliza Mungu.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â