November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sehemu hizi ni hatari kuhifadhi kondom

Na  Aveline Kitomary,TimesMajira Online ,Dar es Salaam

UTUMIAJI wa kondom ni hatua muhimu zaidi kwa jamii kwani huweza kumkinga mtumijia na mgonjwa ya kuambukiza wakati wa ngono.

Kiwango cha utoaji elimu kuhusu matumizi ya kondom ni kubwa ambapo inasisitizwa kukinga magonjwa kama vile UKIMWI,Kaswende,Kisonono   na magonjwa mengine ya kuambukiza.

Lakini sio hilo tu hata katika kampeni ya uzazi wa mpango matumizi ya kondom yanatajwa kama njia mojawapo  y akumuepusha mtumiaji na mimba zisizotarajiwa.

Ni hatua muhimu zaidi kuzingatia matumizi ya kondom ambapo kundi kubwa la vijana elimu hiyo imewaingia vizuri.

Matumizi ya kondom ni  hatua nzuri lakini je watumiaji wanaelewa njia  ya kuhifadhi bidhaa hiyo isiweze kupoteza ubora wake?

Jarida la Majira ya Afya  lilifanikiwa kupita kati maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na kuzungumza na vijana ambao ni watumiaji wakubwa wa bidhaa hizo.

 Katika mahojiano na vijana  hao Mwandishi wa makala hii alipouliza  kama wanaulewa kuhusu namna bora ya kuhifadhi kondom wengi wasisema hawajui.

“Mimi ni mtumiaji mzuri wa kondom  lakini kuhusu uhifadhi hilo bado sijalijua ,huwa nanunua kondom na naweka hata mwezi mmoja na mara nyingi natembea nzno kwasababu naamini kuwa ni ulinzi kwangu.

“ninachokiangali katoka kondom ni muda wa matumizi ukiisha basi naitupata lakini kwa upande wa njia ya kuhifadhi naweza kuweka mfukoni nikatembea nayo au naweka kwenye wallet,”anaeleza John  Koluwu kijana mwenye umri wa miaka 24.

Sio John tu  hata  Obedi anasema kwake kununua kondom na kukaa nayo muda mrefu ni jambo la kawaida na wakati mwingine kutembea nayo.

“Lazika geto kwangu niwe na kondom kwasababu wakati mwingine mpenzi wangu akija atataka tutumie  hivyo naiweka kama akiba.

Alipoulizwa kuwa ni njia gani anatumia kuhifadhi kondom isipoteze ubora anasema “Sijui hilo kuwa kondo inaweza kupoteza ubora na hata namna ya uhifadhi wake siujui mimi nikinunua dukani tu basi.

“Lakini ninachoamini hata vijana wengi hawajui hilo lakini kuna wengine hata expire date hawaangali nafikiri kuna haja ya kulielewa hilo,”anasema Obedi.

Anaongeza “wakati mwingine utakuta wapo wanaoshea kondom moja akitumia huyu anaweza kumpa mwenzake akatumia hilo nilishawahi kusikia.

“alakini hata ukinunua unakuwa haumalizi kutumia zpte kwahiyo zinazobaki zinakaa na kuwa akiba.

Mchunguzi wa maabara wa TMDA, Samson Mwambene akionesha jinsi maabara yao inavyochunguza ubora,ufanisi na uwezo wa kondom

HAZITAKIWI KUHIFADHIWA  SEHEMU HIZI

Watumiaji wengi wa bidhaa za kondom hupenda kuzihifadhi katika mifuko ya suruali,droo za kabati  au wallet zao kwa muda mrefu.

Hali ya kutembea nayo muda mrefu hasa kwenye mwanga wa jua na joto kali inaweza kuwa na hatari kubwa kwa mtumiaji.

Mchunguzi wa Maabara wa Mamlaka ya Dawa,Vifaa tiba na Vitendanishi (TMDA) Samson Mwambene anafafanua hapa  “Tunahofu na kitu ambacho sio kizuri tukumbuke mazingira  tunayotakiwa kuhifadhi  kwanini uweke kondom kwenye waleti halafu unazunguka nayo mtaani na juani unazurura ni rahisi sana ikikutana na jua unatumia kondom haina ubora.

“Kuna wakati unakuta mtu analalamika kondom inapasuka kumbe ni namna anavyohifadhi mwingine ananunua leo anaenda kuiweka mahali sio salama inapata jua kondom inaharibika.

Kwa mujibu  wav Mwambene anasema ni muhumi kuzinagatia uhifadhi wa kondom ili kulinda ubora wake na kufanya kazi kwa ufanisi.

Mwambene anasema kiwango cha juu cha  joto kinachotakiwa katika uhifadhi wa kondom ni nyuzi joto 30 huku kiwango cha chini ikiwa ni nyuzi joto 10.

“Kiwango cha joto hakitakiwi kuzidi 30 sio vizuri kuweka kondom kwenye droo au sehemu yenye joto Unaweza kuhifadhi katika mazingira ya joto la chini  10 hadi 30.

“Unapoenda kununua kondom usiende kila mahali nenda sehemu kuna maduka ukiingia unahisi hali ya ubaridi unaona kimehifadhiwa vizuri kama unyevu uko juu itaharibu na pia kama joto iko juu itaharibika na hii ni kwa dawa na vifaa tiba pia.

“Kama kunakitu chenye madhara makubwa ni kutumia kondom na kufua na kuitumia tena madhara yake ni makubwa ukishatoa kwenye boksi kubwa halfu vidogo na kwenye pakiti haitakiwi kukaa muda wa dakika mbili,”anasisitiza.

Anasema mtu anapoifungua kondom anatakiwa aitumie muda huo huo na ikiachwa kwa dakika mbili inapoteza ubora wake.

“Tunashauri ukishafungua iwe tayari kwa matumizi sio unafungua ukaiweka hafu ukazunguka unakaja kuitumia au unatumia unaenda kusafisha na kuitumia tena.

“Tunasema kondom inatakiwa kuwa na mafuta kama utafua itakuwa kavu na itachanikana na kama haina mafuta oksijeni itakuwepo na ubora utakuwa haupo vizuri ,Hatushauri kabisa kutumia kondom ambayo imeshatumika,”anabainisha.

Anashauari kondom kuhifadhiwa sehemu salama.

 “Kutembea na kondom ni kinga lakini unazingatia uhifadhi salama hicho ni muhimu isikutane na mwanga wa jua wala joto kali,”anasisitiza Mwambene.

ELIMU NI ENDELEVU

Kwa upande wake Meneja Mawsiliano na Elimu kwa Uma wa TMDA,Gaudensia Simwanza anasema mamlaka inaendelea kutoa elimu kwa watumiaji ili kujua namna bora ya kuhifadhi vifaa tiba ikiwemo kondom.

“Tunatoa elimu katika sehemu mbalimbali na hilo ni suala endelevu tunataka jamii kuwa na uelewa kuhusu hilo,”anasema Simwanza.

UPIMAJI UBORA KATIKA MAABARA

Mwambene anasema  maabara ya TMDA inachunguza uwezo,ufanisi na ubora wa kondom za kike na kiume kabla ya kuingia katika soko.

Anasema zipo mashine za kisasa ambazo zinauweza wa kuchunguza kondom kwa kuangalia  matundu,urefu,upana na kiwango cha mafuta kilichopo.

 “Kuna mashine inaitwa Electrical  leak  tester(ELT)  Kazi yake kwaajili ya kuchunguza mashimo madogo  ambayo yanaweza yakawa kwenye kondom kwani  zile kondom wakati wa uzalishaji unaweza kuenda tofauti vile ambavyo intarajiwa hivyo inatengeneza vishimo vidogo ambavyo hatuwezi kuziona kwa macho  lakini wakati wa usafishaji  hiyo inaweza kutokea na wakati wa utunzaji  inaweza kutokea.

“Kwahiyo procees za uchunguzi zinaanza kufanyikia  kiwandani inapozalishwa halafu sisi tunathibitisha ubora wa kile tunacholetwa kama inakidhibi ubora.

“ Kwasababu katika maelezo yao wanasema ni bora, hivyo tunathibitisha  vipi sasa mashine hii inatusaida kuchunguza vitundu vidogo sana na yenye inauwezo  wa kuchunguza kutumia umeme,”anaeleza.

Anasema katika mashine hizo kuna taa ambazo zinawaka kujulisha kama ni salama ua sio salama .

 “Taa ikiwaka ya  njano inaonesha kuna shida katika hiyo kondom na kukiwa hakuna shida zinawaka taa za kijani kuonesha kuwa hakuna tatizo.

 “Tunaingiza maji kwenye kondom ambapo umeme unapita maji hayo sodium chloride ,Kama kondom haina tatizo la tobo itaonekana na kama inatatizo itaonesha sehemu Fulani inatatizo.

“Ili kuthibitisha kuwa toleo zima zilifeli au zimefauli  katika kondom 315 tutakazo pima inatakiwa ziwe mbili tu zilizofeli kama ni zaidi ya mbili maana yake toleo zima linakuwa limefeli,”anabainisha.

Anasema toleo  mara nyingi zinazalishwa kwa viwango tofautitofauti huku  wengine ikiwa ni 500,000  na wengine  chini ya 500,000.

“Kama ikotokea tukaruhusu kuingia mtaani ikiwa haijathibitishwa inaweza kuwa na madhara makubwa kwa jamii ,Wakati wa tendo msuguano unapotokea tundu litaruhusu kutoka majimaji ni hii itahatarisha maisha ya mtumiaji.

KUCHUNGUZA MAFUTA

Mwambene nasema  kondom inaweza kuharibiwa na oksijeni hivyo inavyotengenezwa inawekwa mafuta (lubricant).

“Halafu wanaweka kwenye  pakiti  yakena wakati mwingine inatokea ile  kifungashio  walivyokuwa wanafungasha hawakufungasha  vizuri kwahiyo yale mafuta yanatoka madhara ya kutoka yale mafuta yanasababisha vitu viwili .

“Kitu cha kwanza ile kondom itaanza kuharibika   na adui wake mkubwa  ni oksije itaanza kuharibu  ile kondom .

“Cha pili  ile lubricat  ina potoka inaenda kuchafua vifungashio  vingine hata kujua ni ipi inakuwa ni changamoto kwasababu  mafuta yameshatoka na imeleta  uharibifu kwenye  vifungashio vingine

“mashine ya Visual Leak Tester (VLT)  inaweza kutambua kama hii haijakaa vizuri, baada ya oksijeni kuharibu kondom na ukaenda kutumia  inaweza kuchanikachanika  kwasababu ubora haupo tena.

“Mfano  mtu kaifungua  kondom halfu kaiacha mahali iko kwenye pakage halafu baadae anatumia mafuta yanakuwa yametoka na kuwa kavu yale mafuta yanasaidia wakati wa tendo  kulainisha na mafuta yakishatoka ikitumika inaweza kuchanika kwasababu ya msuguano itapasuka ,”anaeleza Mwambene.

Anasema  Kazi ya mamlaka ni kuhakikisha bidhaa kuwa  bora na  mtanzani yuko salama  hivyo  inachunguzwa kwa umakini na wataalamu waliobobea.

“Bidhaa zilizoko katika soko pia zinafatiliwa ubora wake na kama tutakuwa na wasiwasi zitatolewa

Tunaangali kwamba kifungashio haina tatizo.

“Katika kuangali  kiwango cha mafuta tunaangali sample 32 tu na katia hizo hazitakiwi kufeli zaidi ya mbili kama ikifeli toleo zima tunaliweka kwenye nkiulizo

“ kwani Matumizi ya kondom isiyo na ubora ni hatari sana kwani inaanza kumuangamiza mtu mmoja halafu familia na taifa, tukishapama maangamizi ya virusi au magonjwa ya zinaa au kuzuia mimba matokeo yake  yanaenda mbali hivyo tuko makini zaidi katika kuchunguza.

“Kwahiyo inachunguzwa mara nyingi na watu tofauti tofauti hatuwezi kufanya uzembe kwasababu athari yake ni kubwa kwa watumiaji ,tunafatilia hadi mtaani kuwa watu wakilalamika kuwa hii inashida itakusanywa na italetwa kufanya uchunguzi halafu toleo husika litatolewa sokoni ,”anafafanua.

MUHIMU KUANGALIA MUDA WA MATUMIZI

Mwambene anasema Kifaa  chochote inapopita muda wa matumizi  huwa inakuwa na madhara endapo itatumiaka.

“Muda wa matumizi ukiisha inakuwa tayari sio salama kwa matumizi  ni kitu muhimu sana mtu anatakiwa kunagalia muda wa matumizi kabla hajanunua bidhaa ,muda wa matumizi ukiwa umekaribia kama mfano umeenda kununua bidhaa Novemba na inakufa disemba nashauri kabisa usinunue kwanini ujiweke katika hatari .

Simwanza anasema kuna wakaguzi katika maeneo mbalimbali  kuangalia bidhaa ambazo wanapima .

 “Kama sampo  iliyoharibika iko mtaani tutawasiana na mtengenezaji halafu itatafutwa nchi nzima na kuitoa soko ,Tunatoa taarifa kwa umma tunawaita tunawaeleza kuwa kuna toleo tumelitoa sokoni,”anasema Simwanza