Na Netho Sichali, TimesMajira online,Nyasa
MKUU wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba amewataka wataalamu na viongozi kuanzia ngazi ya vijiji, kata na Halmashauri kusimamia zoezi la uhakiki wa wanufaika wa TASAF kipindi cha pili ili rejesta/orodha ya wanufaika wanaostahili.
Ameyasema hayo jana katika Ukumbi wa Kap.John Komba wakati akifungua kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Kipindi cha Pili kwa Viongozi, Watendaji na Wawezeshaji katika Ukumbi wa Kapten John Komba Mbamba bay Wilayani hapa.
Chilumba amefafanua kuwa madiwani ni viongozi ambao wako karibu na wananchi, hivyo amewataka mafunzo wanayopewa wakayatumie kushirikiana na wawezeshaji ili kupata wanufaika wanaostahili na kuacha siasa katika zoezi la uibuaji walengwa hao.
Ameongeza kuwa mpango wa kunusuru kaya maskini kipindi cha pili kinawataka viongozi hao kuwa waaminifu na waadilifu, ili kuondokana na malalamiko ya wananchi ambao watakuwa wanalalamika endapo watachukuliwa wasio na sifa na kuachwa wenye sifa.
Ametoa wito kwa wataalamu na viongozi hao kusikiliza mafunzo kutoka kwa wawezeshaji ambayo yatawajengea uwezo wa kutekeleza vema majukumu katika maeneo yao.
Awali akitoa maelezo mafupi ya kuhusu kikao kazi mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw.Salumu Mshana amesema atamchukulia hatua Mtendaji yeyote atakayeibua walengwa hewa katika eneo lake atakalopangiwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imefanya kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu Mpango wa kunusuru kaya maskini Kipindi cha pili kwa Kamati ya Ulinzi na usalama wilaya ya Nyasa, Madiwani, Wakuu wa Idara na Vitengo na Watendaji na Wawezeshaji.
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Watu 5,000 kuhudhuria tamasha la utamaduni Songea