November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamonga achukizwa na usimamizi mbovu Chuo cha Veta Ludewa

Na David John, Timesmajira Online, Njombe

MBUNGE wa Jimbo la Ludewa Mkoani Njombe Joseph Kamonga amesema utendaji mbovu na usimamizi mbaya wa Ujenzi wa chuo cha Ufundi VETA Wilayani humo umechelewesha kukamilika kwa ujenzi wa Chuo hicho.

Uzembe huo umepelekea hadi wafadhili wa mradi kutoka ‘African Development Benk’ kujitoa katika ujenzi huo hali iliyochangia wananchi kukosa haki ya kupeleka watoto wao kupata ujuzi kama ilivyokusudiwa na Serikali.

Kamonga ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara ya kushutikiza akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubrya katika Kijiji cha shauli moyo unapotekelezwa mradi huo ambapo amewaeleza wananachi wa eneo hilo kwamba yeye kama Mbunge amesikitishwa na ucheleweshwaji huo wa ujenzi wa chuo hicho.

“Ndugu zangu Rais Dkt John Magufuli alitoa fedha kupitia ufadhili wa African Development Benk (ADB) lakini kutokana na uzembe wa usimamizi wa watendaji umesababisha wafadhili kujitoa na kukiacha chuo kutokamilika hadi leo,” amesema Kamonga.

Amesema, baada ya VETA kushindwa kusimamia mradi huo, hivi sasa mradi unafanywa na Wizara ya elimu kupitia Chuo cha ufundi ambapo kwa kuanzia wametoa

shilingi bilioni 2 kati ya bilioni 6 ambazo zitagharimu mradi huo hadi kukamilika kwake ambazo atahakikisha anasimamia mradi huo hadi utakapokamilika.

“Ndugu zangu nataka niwaambie kuwa mradi huu umechelewa kutokana na uzembe wa baadhi ya watendaji na kusababisha aliyekuwa mfadhili kujitoa lakini leo hii ndio manaa mmeona tupo hapa na mkuu wetu wa mkoa Mhandisi Marwa Rubrya ili kuona maendeleo yake,” amesema Kamonga .

Amesema, baadhi ya wananchi walitoa maeneo yao ili kuhakikisha Chuo hicho kinajengwa lakini kwa bahati mbaya watu waliokuwa wanasimama wamekwamisha ujenzi huo lakini amewaomba wananachi kutulia .

“Lengo la kuanzisha Chuo hiki ni kuwapa fursa vijana wetu ambao wanashindwa kwenda Sekondari kupata mafunzo ya Ufundi Stadi ili kuweza kupata ujuzi.”amesema Kamonga .