November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge wa jimbo la mbeya mjini na Naibu Spika Dkt.Tulia Akson akiongea na wananchi wa jimbo lake .

Dkt.Tulia awatoa hofu wananchi wa kata tatu ujenzi wa kivuko

Na Esther Macha,Timesmajira, Online,Mbeya

MBUNGE wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt.Tulia Ackson amefanya ziara ya ukaguzi wa Ujenzi wa kivuko cha relini kinachounganisha barabara ya kata za Tembela, Mwasanga na Mwakibete ambacho kimekuwa kero kwa muda mrefu kwa Wananchi wa kata hizo .

Dkt .Tulia amesema kuwa wananchi wa kata hizo kipindi cha mvua hukosa mawasiliano ya barabara baada ya daraja kuu lililokuwa likitumika kuvunjika miezi kadhaa iliyopita.

Mbunge huyo ameambatana  na viongozi mbalimbali wa chama pamoja na TARURA, na kusema kuwa kipindi cha mvua waliahidi katika kampeni kuwa lazima wapate njia mbadala ya kupata mawasiliano.

“Kwasababu  daraja lililovunjika  halijatengamaa hadi leo na wote ni mashahidi lilisababisha  vifo vya watu, kwahiyo tunaendelea kufuatilia ili kupata mbadala kwasababu mvua zinakaribia tena kuanza”amesema na kuendelea

“Sisi tulianza kwa kutengeneza daraja la muda lakini sio salama sana na ndio maana tumeamua kuja kufuatilia maendeleo ya kivuko hiki mapema kabisa ili tuweze kushughulika nalo na tayari wenzetu TAZARA pamoja na TARURA wameshakubali kutusaidia kuweka mambo sawa ili kivuko na barabara hii iweze kutumika” amesema Dkt.Tulia Akizungumzia kuhusu daraja la awali lililovunjika amesema tayari upembuzi yakinifu umefanyika na tayari limefikia hatua nzuri hivyo wananchi wanapaswa kuondoa hofu kwani daraja hilo linatengenezwa kwa kiwago ili kuweza kusaidia mawasiliano baina ya kata hizi tatu za Tembela, Mwasanga pamoja na Mwakibete