October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Magufuli aapishwa kuwa rais muhula wa pili

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online, Dodoma

RAIS John Pombe Magufuli leo ameapishwa kuwa rais wa Tanzania kwa awamu ya pili baada ya kutetea nafasi yake na kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28,mwaka huu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiapishwa na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili cha Awamu ya Tano leo katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma

Rais Magufuli alishinda kwa kupata kura 12,516,252 ambayo ni asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa. Tundu Lissu kutoka chama cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,933,271 ya kura zote zilizopigwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiapa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kuapa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili cha Awamu ya Tano leo katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU

Rais Magufuli ni rais wa tano kuiongoza Tanzania kuanzia mwaka 2015 mpaka 2020 na sasa anatarajia kuongoza mpaka mwaka 2025.