Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Kisheria ngazi ya Mkoa na Wilaya pamoja na kliniki ya sheria bila malipo kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha.
Tukio hilo linatarajia kufanyika Novemba 24, 2026, katika Uwanja wa FFU, Oljoro, jijini Arusha, kuanzia saa 2:00 asubuhi, likiwa limeandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kupitia kliniki hiyo, wananchi wa Mkoa wa Arusha watapata fursa ya kupata huduma za kisheria bila malipo, huku uzinduzi wa Kamati za Ushauri wa Kisheria ngazi ya mkoa na wilaya ukiwa sehemu nyingine ya shughuli zitakazofanyika katika hafla hiyo.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imetangaza tukio hilo na kuwaalika wananchi wa Mkoa wa Arusha kujitokeza kushiriki katika uzinduzi huo na kliniki ya sheria.

More Stories
Waziri Chande azindua bweni la Wasichana Chuo cha BTI
TTCL yafungua milango ya Kidijitali kwa Watanzania
Bunge la vijana lahitimishwa, vijana wahimizwa uongozi bora