November 12, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Homera ampongeza Rais Samia kwa ajenda ya nishati safi

Na Mwandishi wetu,TimesMajira

Waziri wa Nishati,Juma Homera, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuongoza jitihada za kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini, akisema Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa katika kuendeleza ajenda hiyo barani Afrika.

Waziri Homera ametoa pongezi hizo Novemba 11,2026 wakati akitoa salamu za ukaribisho za Wizara ya Nishati kwa Rais Samia katika Mkutano wa Ngazi ya Juu kutangaza mafanikio ya mpito wa Nishati Tanzania na Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika Shule na Vituo vya Afya, uliofanyika pembezoni mwa COP31 jijini Antalya, Türkiye.

Ameeleza kuwa chini ya uongozi wa Rais Samia, matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini yameongezeka kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi asilimia 28.6 mwaka 2025, hatua inayoonesha maendeleo katika utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia wa 2024–2034.

Mkutano huo uliwakutanisha viongozi wa Serikali, wadau wa maendeleo na taasisi za kimataifa kujadili mafanikio, fursa za uwekezaji na kuimarisha ushirikiano katika kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Tanzania inalenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.