Na Mwandishi Wetu,TimesMajira
KAMPUNI ya Premier Bet imeunga mkono juhudi za uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya jamii kupitia udhamini wa Kitonga Marathon 2026 iliyofanyika Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa.
Udhamini huo ni sehemu ya dhamira ya kampuni hiyo ya kurudisha kwa jamii na kushirikiana na Serikali katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.
Kupitia ushiriki wake katika marathon hiyo, Premier Bet imeungana na Serikali pamoja na wadau wengine kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira, kukuza fursa za kiuchumi na kuchochea maendeleo endelevu katika Wilaya ya Kilolo.
Kampuni hiyo imeeleza kuwa inaendelea kuwekeza katika michezo kwa lengo la kukuza vipaji, kuibua fursa mbalimbali na kutumia michezo kama nyenzo ya kuleta maendeleo na kuunganisha jamii.
Aidha, ushiriki wa Premier Bet katika Kitonga Marathon 2026 unaonesha dhamira yake ya kuwa mdau muhimu katika mipango mbalimbali inayolenga kuleta mabadiliko chanya na manufaa kwa jamii.

Kupitia ushirikiano huo, kampuni inaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau wengine katika kuendeleza michezo, kulinda mazingira na kuboresha maisha ya wananchi.
Kaulimbiu ya kampeni hiyo, “Tunza Mazingira, Wekeza Kilolo,” imebeba ujumbe wa kuhamasisha jamii kushiriki katika uhifadhi wa mazingira huku ikichochea maendeleo endelevu katika wilaya hiyo.


More Stories
Tanzania mwenyeji Mkutano wa IPCC
WWF : Ongezeni juhudi katika kuibua masuala ya uhifadhi wa mazingira
Mawakala zaidi ya 270,000 waongezewa fursa za kipato