Na Mwandishi Wetu,TimesMajira
WAZIRI wa Nishati, Dkt. Juma Zuberi Homera, ameitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuboresha kwa kasi huduma kwa wateja na kuhakikisha malalamiko pamoja na changamoto zinazowasilishwa na wananchi zinapatiwa majibu na ufumbuzi kwa wakati, akisisitiza kuwa kuridhika kwa wateja ni sehemu muhimu ya ufanisi wa shirika hilo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Juma Zuberi Homera, ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mkataba wa huduma kwa wateja uliohusishwa na huduma nyingine za wateja wa Tanesco.
Amesema Tanesco ina wajibu wa kuwa na mifumo imara ya kusikiliza, kuelewa na kutatua changamoto za wateja, akisisitiza kuwa maoni na malalamiko ya wananchi yanapaswa kutumika kama fursa ya kuboresha huduma.
Amesema pamoja na mchango wa Tanesco katika uchumi na mapato ya Serikali, shirika hilo linapaswa kuhakikisha huduma linazotoa zinaendana na mahitaji ya wananchi.

Amesema Tanesco inapaswa kuhakikisha changamoto zinazowasilishwa na wateja zinashughulikiwa kwa wakati, huku shirika likiendelea kuboresha mifumo ya huduma ili kuongeza ufanisi na kurahisisha mawasiliano kati yake na wananchi.
Aidha, Dkt. Homera amelitaka Tanesco kuhakikisha mikataba inayotekelezwa inaendana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya shirika hilo na wateja wakubwa pamoja na wadogo.

“Pamoja na kuangalia mikataba hiyo pia tunatakiwa kutoa muda wa kutosha kwa wateja kuwatatuliwa changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika huduma za umeme,” amesema Dk. Homera
Pia amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha mifumo inayotumika katika utoaji wa huduma inafanya kazi kwa ufanisi wakati wote, akitaka kupunguza urasimu na kuimarisha utendaji wa watumishi wanaohusika moja kwa moja na huduma kwa wananchi.

More Stories
Zungu achaguliwa kuwa Rais wa Mkutano wa 153 wa IPU
Dkt.Homera azindua mkataba mpya wa huduma TANESCO
Yas, Mixx kupeleka huduma kwa wateja masokoni